Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

KATIKA kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendelea kuhamasisha ulipaji kodi wa hiali Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imezindua Ofisi ya walipa kodi binafsi wenye hadhi ya juu ambayo kwa lengo la kuwaondolea usumbufu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi ofisi hiyo Jijini Dar es salaam iliyopo katika jengo la Golden Jubilee Tower,Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda amesema lengo la kufungua ofisi hiyo ni kuendelea kuimarisha huduma za kikodi kwa walipa kodi.

Amesema kundi hilo limebeba walipa kodi ambao mapato yao ni makubwa ikiwemo kumiliki makampuni pamoja na kuajiri watu huku wakilipa Kodi .

Kamishna Mkuu huyo amesema ofisi hiyo itakuwa ikitoa huduma kwa makundi manne ambao ni pamoja wamiliki wa kampuni ambao wanaingiza Sh Bilioni 20 kwa mwaka pamoja na wamiliki wa hisa katika makampuni ambazi zina thamani ya zaidi ya Sh bilioni 2.5, na mtu mwenye ubia na kampuni zinaingiza faida Sh Bilioni 20 kwa mwaka.

Amesema huduma hiyo kwa sasa imeanza na walipa kodi 158 ambapo kati ya hayo wamiliki binafsi wapo 111 wote wameshaitwa kueleshwa kuhusu huduma hiyo,huduma pia itagusa viongozi wa mihimili mitatu ambapo kwa sasa viongozi 47 kutoka ngazi za juu,”amesema

“Ofisi hii ina lengo la kuangalia kodi zao wao sio za makampuni yao …kwaiyo wanaitaji kupata elimu ya kutosha mara kwa mara na kuangalia kile wanachostahili kulipa ni kipi”

Na kuongeza “Huu ni udhibitisho kwamba hawa nao ni wanalipa kodi kama wengine wanavyolipa Kodi .. mfano kama mwajiriwa anavyolipa hawa nao wanalipa kwaiyo kanuni yetu ya mfumo mzuri wa wa Kodi inawataka wenye uwezo mkubwa kama hawa kulipa kodi inayotakiwa.”amesema Mwenda

Aidha alilishukuru kundi hilo kwa mchango wao mkubwa na kuahidi kuwahudumia kwa viwango vya ubora ili wasipate matatizo ya kile wanacholipa na kulipa kinachostahili.

Vilevile amesema kwa upande wa kundi la viongozi wataangalia mapato yao ya shughuli wanazofanya kama vile ajira ikiwemo kuwaangalia kwa ukaribu na kuwashauri ili wachagie kile wanachostahili.

“Nawapongeza sana kwani sio wote waliopata hadhi hii ..tunawapongeza sana pia tunawahakikishia huduma nzuri sio tu zinazohusiana na mapato yao lakini pia za makampuni yao hata za shughuli zao nyingine za Forodha, elimu”amesema Mwenda

Amesema TRA itaendelea kutoa elimu ya mara kwa mara ili kuwawezesha kupata wanachostahili na kulipa wanachostahili.

Hata hivyo amesema huduma hiyo sio mpya kwao na kueleza kuwa walikuwa wakilipa katika Udala ya walipa kodi wakubwa, wa kati, wadogo, na hivyo wameamua kuwaleta pamoja ili wapate huduma zinazoendana na wao.

“Tutakuwa tukiwaangalia kwa ukaribu kwa kile wanachostahili kulipa wakilipe ili wasije kupata matatizo baadae “alisisitiza Mwenda

Aidha amesema kuanzishwa kwa ofisi hiyo sio kuwataka walipe kodi kubwa sana bali walipe kinachostahili sambamba na kupewa elimu itakayorahisisha shughuli zao ili wapate muda wa kwenda kutafuta pesa zaidi.

Please follow and like us:
Pin Share