Na Richard Mrusha, JamhuriMeia, Dodoma

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imejipanga kutatua kero za kikodi kwa wananchi waliokutana na changamoto mbalimbali.

Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na wavuvi yanayoendelea Jijini Dodoma.

Mwenda amesema, “ili eneo ni moja ya eneo ambalo tutachukua changamoto za kikodi za walipa kodi na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.

“Kwa hiyo nitoe wito waje waonane na watu wetu waeleze wanachokihitaji wapate elimu,” amesema.

Pia amesema TRA imejipanga kuhudumia walipa kodi kwa haraka , mwisho waweze kuchangia.

Awali aliwataka watanzania waliofikia kiwango cha kulipa kodi , wafike katika banda la TRA ili waliopo wapate elimu ya kodi, mabadiliko ya sheria na pia ikiwa ni pamoja huduma za kuwakadiria kiasi.

Please follow and like us:
Pin Share