Na Happy Lazaro, JamhuriMedia, Arusha

MAMLAKA ya afya ya mimea na viatilifu Tanzania (TPHPA) kwa kushirikiana na Taasisi ya udhibiti wa kemikali ya nchini Sweden(KEM) wamesaini hati ya makubaliano ya kuendeleza mashirikiano ya pamoja katika utendaji kazi zao .

Aidha makubaliano hayo wamesaini katika maeneo matatu ambayo ni pamoja na kuendelea kushirikiana katika udhibiti wa viatilifu ili kulinda afya ya walaji pamoja na mazingira,kuendeleza na kutengeneza miongozo mbalimbali kwa ajili ya udhibiti wa viatilifu ,na kuangalia matumizi ya mifumo ya kimataifa katika kutambua kemikali.mbalimbali pamoja na kuweka label zake .

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusaini makubalino hayo ofisini kwake.

Aidha amesema kuwa, mashirikiano hayo ni mwendelezo kwani wamekuwa na mashirikiano kati yao na Taasisi hiyo ambapo katika mashirikiano hayo wataalamu kutoka TPHPA wamekuwa wakienda kupata mafunzo nchi ya Sweden ya namna mbalimbali ya kudhibiti matumizi ya viatilifu na pia nao wamekuwa wakija hapa nchini kushirikiana na sisi pamoja na Taasisi zingine mbalimbali hapa Tanzania katika kufanya utafiti wa viatilifu hai katika kudhibiti visumbufu mbalimbali vya mazao .

“Ushirikiano huu ni mzuri kwani malengo ya mamlaka ni kuleta tija hasa katika kilimo pamoja na kulinda afya ya walaji,wanyama na mazingira kwa kuwa na matumizi sahihi na salama ya viatilifu kwa hiyo ili.ni jambo zuri kwa leo hii kwa kusaini hati hii ya makubaliano pamoja na wenzetu wa Sweden .”amesema .

Aidha amesema kuwa matarajio baada ya kusaini makubaliano hayo ni kuhakikisha tija inaongezeka katika kilimo,na matumizi sahihi ya viatilifu katika kudhibiti visumbufu pamoja na kupungua kwa athari hasi za viatilifu katika mazingira pamoja na kulinda afya ya binadamu na kujengeana uwezo wa watalamu wetu katika tasnia nzima ya matumizi sahihi na salama ya viatilifu hapa Tanzania .

Amefafanua kuwa,ili uweze kufanikiwa na kufika mbali lazima mashirikiano yawepo baina ya Taasisi moja na Taasisi nyingine kwani wana maono makubwa ya kutaka kuona taasisi hiyo inakuwa taasisi mahiri ya kudhibiti maswala yote ya afya ya mimea na viatilifu Tanzania na ili tuweze kufika hapo lazima tushirikiane na taasisi zingine ,kwa kufanya hivyo tunaweza kujipatia rasilimali ya ziada kwa ajili ya kuongeza rasilimali kwani huwezi kutegemea serikali peke yake na hayo ni malengo ya serikali kuhakikisha mashirikiano yanakuwepo.

Kwa upande wake Msimamizi wa mradi kutoka KEM , Raphael Mwezi amesema kuwa mashirikiano hayo.yalianza tangu mwaka 2018 ambapo TPHPA pamoja na Taasisi ya Sweden ziliingia kwenye mashirikiano ya kudhibiti sumu ambapo wamefanya mengi ikiwemo kubadilishana uzoefu kupatiana mafunzo na kupeana mbinu za uzoefu kati ya usimamizi wa viatilifu.

‘katika.mashirikiano hayo tuliendelea hadi kufikia mwaka 2023 hadi 2024 ambapo waliona kuna umuhimu wa kuingia kwenye makubaliano haya mapya .”amesema .

“Leo katika makubaliano hayo tumekubaliana mambo matatu ikiwemo kupeana uzoefu kwenye mambo ya mafunzo ,utendaji kazi,pamoja na usimamizi wa mikataba ya kimataifa pamoja na uwezo wa usimamizi wa viatilifu ikiwemo mfumo mzima wa kuweka vibandiko na usajili pamoja na vitu vyote vinavyohusiana na usimamizi wa viatilifu .”amesema Mwezi .

Kwa upande wake Meneja katika kitengo cha usimamizi wa teknolojia ya unyunyuziaji wa viatilifu (TPHPA) Dk Magreth Francis amesema kuwa , kuwa,wamefurahi sana kushirikiana na KEMI kwani moja ya majukumu.yao.katika kitengo wanatamani sana kuwafundisha wakulima juu ya matumizi sahihi ya viatilifu yenye lengo la kumlinda binadamu pamoja na mazingira pamoja kuhakikisha wanapata mazao yaliyo masafi kwa ajili ya soko la nje na la ndani.

Amesema kuwa, mashirikiano hayo yatakuwa ya muhimu sana kwao kama.watapata uwezeshaji kutoka kwao maana watawawezesha kuwafikia wakulima kuwafundisha matumizi sahihi pamoja na upimaji wa afya hasa kwa watumiaji wa viatilifu na kupata majibu mazuri namna sahihi ya matumizi ya viatilifu.