Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia,Dodoma
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema tangu Serikali ya awamu ya Sita iingie madarakani,mapato ya mamlaka hiyo yameongezeka kutoka shilingi trilion 1.1 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi shilingi trilion 1.475 Mwaka wa Fedha 2023/24.
Hayo yameelezwa leo jijini hapa February 24,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa TPA Plasduce M. Mbossa wakati akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Mamlaka hiyo (2021/22 – 2023/24) ikiwa ni mafanikio ya Mamlaka hiyo tangu Serikali ya awamu Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan iingie madarakani.
Amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/23 mchango wa sekta ya bandari ulikuwa Shilingi trilioni 10.8 sawa na asilimia 7.3 ya pato la Taifa lililokuwa Shilingi trilioni 148.3.
“Ongezeko hili la mapato limetokana na:
Mapato ya matumizi ya bandari kuongezeka kutokana na ongezeko la shehena iliyohudumiwa bandarini mapato ya kuhudumia meli ambayo yameongezaka kutokana na ongezeko la idadi ya meli na ukubwa wa meli.

Mapato ya mrabaha kwa tani au kasha linalohudumiwa na Kampuni ya DPW Dar es Salaam na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEGTL) pamoja na tozo la pango (Lease Rent) la maeneo ya bandari iliyolipwa na kampuni hizo kwenda Serikalini kupitia TPA, “amesema.
Akizungumzia kuhusu utendaji wa kipindi cha Julai-Desemba, 2024 katika kipindi cha miezi sita ya Mwaka wa Fedha 2024/25 (Julai-Desemba, 2024)amesema jumla ya Shehena iliyohudumiwa na Bandari za TPA ni tani milioni 15.49 ambayo imezidi lengo lililowekwa la kuhudumia tani milioni 14.60 kwa asilimia 6.1, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 11.1 ikilinganishwa na tani milioni 13.94 iliyohudumiwa kipindi kama hiki mwaka uliopita (Julai-Desemba, 2023).
Amesema jumla ya Shehena ya Makasha iliyohudumiwa na Bandari za TPA ni Makasha TEUS 565,361, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 4.9 ikilinganishwa na shehena ya Makasha TEUS 539,013 iliyohudumiwa kipindi kama hiki mwaka uliopita (Julai-Desemba, 2023).
Mkurugenzi huyo pia amesema kuwa mamlaka hiyo ikiwa na dhamana ya kutangaza Bandari kimasoko (Promote),
Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Bandari (Safety and Security),
Kushirikisha na kusimamia Sekta Binafsi katika uendeshaji wa shughuli za Bandari (Landlord)kwa sasa ina simamia Bandari rasmi 131 zilizoko katika Bahari ya Hindi na Maziwa Makuu.
“Katika Bahari ya Hindi kuna bandari 32 na katika Maziwa Makuu kuna bandari 99,ili Kurahiisisha biashara, TPA imefungua ofisi katika nchi zisizo na Bahari ikiwemo
DRC (Lubumbashi) 2014,Zambia 2015,Burundi2017, Rwanda 2017,Uganda 2022,DRC (Kolwezi) 2023,Malawi 2023 na Zimbabwe 2023.
Akizungumzia hali ya utendaji wa TPA amesema imeboreka ambapo
Jumla ya Shehena iliyohudumiwa
Katika kipindi hiki jumla ya shehena iliyohudumiwa na TPA imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa asilimia 15.23 kwa mwaka kutoka tani milioni 20.78 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi tani milioni 27.55 Mwaka wa Fedha 2023/2024.
“Jumla ya shehena iliyohudumiwa katika Bandari ya DSM iliongezeka kwa wastani wa asilimia 13.38 kwa mwaka kutoka tani milioni 18.67 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi tani milioni 23.98 Mwaka wa Fedha 2023/2024,ongezeko la shehena limetokea baada ya Serikali ya Awamu ya Sita kukamilisha miradi mbalimbali ya ujenzi na maboresho ya miundombinu ya Bandari nchini ikiwa ni pamoja na kukamilisha mradi wa maboresho na uendelezaji wa Bandari ya Dar es Salaam ,”amefafanua.

Mbossa amesema Shehena ya Makasha
Jumla ya shehena ya Makasha (Containers) iliyohudumiwa imeongezeka kwa wastani wa asilimia 12.9 kwa mwaka kutoka makasha (TEUs) 823,404 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi makasha (TEUs) 1,050,486 Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Aidha, jumla ya Shehena ya Makasha iliyohudumiwa katika Bandari ya DSM imeongezeka kwa wastani wa asilimia 10.7 kwa mwaka kutoka makasha (TEUs) 816,368 Mwaka wa Fedha 2021/22 hadi makasha (TEUs) 998,872 Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Amesema ongezeko la makasha katika Bandari ya Dar es Salaam limetokana na maboresho ya uendeshaji wa vitengo vya makasha vya Bandari ya Dar es Salaam kwa kuviweka chini ya uendeshaji wa Sekta Binafsi wa Kampuni ya DP World Dar es Salaam na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL) ambazo zimewekeza kwa kufunga mitambo ya kisasa ya kuhudumia shehena pamoja na mifumo ya kisasa ya TEHAMA ya uingizaji na uondoshaji wa makasha bandarini.
Amesema ili kuongeza maboresho zaidi,Serikali kupitia TPA iliingia mikataba ya ushirikishaji na usimamizi wa sekta binafsi kwa ajili ya kuendesha Bandari ya Dar es Salaam ili kuongeza ufanisi katika bandari hiyo.
“Shughuli za uendeshaji wa Kitengo Na. 1 cha Bandari ya Dar es Salaam gati
Shughuli katika kitengo hiki zilianza kukabidhiwa kwa awamu kwa Kampuni ya DP World Dar es Salaam mwezi Aprili 2024,Kampuni ya DP World Dar es Salaam inaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Uwekezaji ambao unakusudiwa kugharimu kiasi cha Dola za Marekani (USD) 250 Milioni (sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 675) kwa kipindi cha awali cha Mkataba cha Miaka mitano, “amesema
Amesema hadi sasa, Kampuni ya DP World imefanya uwekezaji wa awali katika maeneo mbalimbali ya uendeshaji ili kuboresha na kuongeza ufanisi wa huduma za bandari ambalo ni dhumuni kuu la kuingiwa kwa Mikataba kama ilivyoelezwa hapo awali.
Pia amesema Uwekezaji wa awali uliogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 214.42 umefanywa katika maeneo mbalimbali ikiwemo ununuzi na usimikaji wa mitambo krini za kisasa za kuhudumiwa shehena ya makasha uliogharimu Shilingi Bilioni 115.80 na Ununuzi na usimikaji wa mitambo nane inayotambulika kama “Rubber Tyred Gantry Crane-RTG” katika Gati Na. 1 la makasha la Bandari ya Dar es Salaam iliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 96;
Ununuzi wa ‘terminal tractors’ ishirini (20) ambazo hutumika katika kuhamisha na kusafirisha shehena kutoka eneo moja la bandari kwenda eneo jingine .

Vilevile amesema Serikali ya Awamu ya Sita kupitia TPA inaendelea kutekeleza mapendekezo ya mpango kabambe ya maendeleo ya bandari nchini (2020 – 2045) na programu ya uboreshaji na uendeshaji wa bandari ambao ni mpango wa kitaifa (National Projects Management Information System – NPMIS) ambayo ilisajiliwa Oktoba, 2023 kwa jina la Tanzania Ports Development and Management Programme na kupewa namba ya mradi 4300.
“Katika Programu hiyo Serikali kupitia TPA itaenda kutekeleza miradi 10 ya kimkakati ikiwemo ya kupokelea na kuhifadhia mafuta SRT ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 17 na unagharimu dola za kimarekani million 265,Mradi huu ukikamilika utapunguza siku za kuhudumia meli zenye ujazo wa 150,000 DWT kutoka siku kumi (10) mpaka tatu (3),”amesema.
Ametaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa kituo cha reli na mtandao wake ndani ya bandari ya Dar es Salaam na unagharimu dola za kimarekani million 119.955 na kwamba ukikamilika utapunguza kiwango cha asilimia 98 cha shehena inayotoka bandarini kwa kutumia njia ya barabara na kupelekea kutatua tatizo la msongamano wa malori ndani na nje ya bandari.
“Mradi mwingine ni wa Ujenzi wa gati mbili zenye jumla ya urefu wa mita 500 ambao utagharimu dola za kimarekani million 250,Mradi huu ukikamilika utawezesha ufungaji wa meli mbili zenye ukubwa wa 50,000 DWT katika gati hizo kwa wakati mmoja, ” Amesema