Na Stella Aron, JamhuriMedia, Dar es Salaan

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Nchini (TMDA), Adam Fimbo amewataka waratibu wa Ufuatiliaji Usalama wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi wameshauriwa kutoa taarifa za matukio na madhara ya vifaa tiba na vitendanishi ili taarifa hizo zifanyikazi na kutolewa mrejesho.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 14, 2024 jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Udhibiti na Vfaa Tiba na Vitendanishi Bryceson Kibassa ambaye alisoma risala kwa niaba ya Mkurugenzi TMDA wakati wa mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na TMDA kwa kushirikisha waratibu kutoka mikoa miwili ya Dar es Salaam na Pwani.

Amesema kuwa hayo ni mafunzo ya kwanza kufanyika kwa waratibu hao ambapo ni kuwajengea uelewa na uwezo katika eneo la ufuatiliaji usalama wa vifaa tiba na vitendanishi.

“Nyinyi ndio mmekuwa mkipokea na kukusanya taarifa za matukio na madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi na kuwapatianyenzo za kufanyiakazi ili taarofa zinazowasilishwa TMDA ziwe zimekamilika na kufanyiwa tathmini.

“Hivyo katika mafunzo haya mtajifunza juu a udhibiti wa vfaa tiba na vitendanishi wa ujumla. Hususan mtafundishwa jinsi na jia mbalimbali zitumikazazo na TMDA katika kufuatilia usalama yakiwemo matukio na madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa hizi na kuyatolewa ufafanuzi” amesema

Ameongeza kuwa jukumu la udhibiti wa vifaa tiba lilikabidhiwa rasmi kwa iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mwaka 2008 na udhibiti wa vitendanishi mwaka 2017 hivyo udhibiti wa bidhaa hizi haukuanza zamani sana kama ilivyo kwenye upande wa dawa.

Amesema kuwa pamoja na majukumu mengine ni kufuatilia taarifa za matukio na madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa na vitendanishi lengo ni kufanya ufuatiliaji huu ni kutumiza dhima ya TMDA ya kulinda afya ya jamii kwa kuwakinga wagonjwa na watumiaji wasipate athari zinazotokana na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi vibovu.

“Vilevile ufuatiliaji huu unaiwezesha TMDA kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti ikiwemo kuviondoa katika soko vifaa tiba na vitendanishi duni na vyenye madhara” amesema.

Pamoja na jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na TMDA katika kuelimisha jamii na kufanya uhamasishaji kwa watoa huduma za afya, taarifa za matukio na madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi zinazopokelewa ni chache sana.

“Kumekuwa na ongezeko la utoaji taarifa mpaka 254 lakini taarifa hizi ni chache ukilinganisha na idadi na wingi wa matumizi ya vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini” ameongeza.

Amesema kuwa kutokana na mafunzo hayo anaamini kutakuwa na ongezeko la utoaji taarfa za matukio na madhara ya vifaa tiba na vitendanishi hivyo ni vyema kutumia vizuri fursa hiyo hasa ikizingatiwa kuwa lengo la TMDA ni luongeza upatikanaji wa taarofa hizi ili hatua za kiudhibiti ziweze kuchukuliwa na vfaa toba na vtendanishi visivyofaa na vyenye madhara viondolewe katika soko.

Naye Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw. Adonis Bitegeko amesema kuwa ili kutambua kuwepo kwa vifaa tia visivyokidhi viwango hivi sasa kwa kila kituo cha kutoa huduma kuna fomu za rangi ya chungwa ambazo hutumika kutoa taarifa pindi mgonjwa anapohudumiwa na kupata changamoto kutokana na matumizi ya vifaa tiba ama dawa.

“Utoaji wa taarifa za wagonjwa ama watumishi kupata changamoto ya matumizi ya vifaa tiba visivyokidhi viwango ni mdogo hivyo kupitia karatasi hiyo ambayo mgonjwa atajaza pindi atakapopata changamoto iwe ya kushonwa na nyuzi kisha kukatika ama kutumia kifaa tiba chochote na kupata changamoto atatakiwa kujaza fomu hiyo au kutoa taarifa kupitia simu yake ya mkononi kwa kuingia kwenye ukurasa wetu mitandano ili na sisi tuweze kufanyiakazi changamoto hizo na kuzitolewa ufafanuzi” alisema.

Alisema kuwa utoaji wa taarifa hizo si kwa wagonjwa tu bali hata kwa watumishi pindi wanapopata changamoto kwani Serikali imekuwa ikifanya kila jitihada za kuboresha huduma za afya na kutumia gharama kubwa hivyo kitendo cha watumishi kushindwa kutoa taarifa, TMDA itashindwa kutambua changamoto zilizoko kwenye vifaa tiba na tendanishi.