Na MWandishi Wetu, JamhuriMedia

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk. Ladislaus Chang’a, amewaonya wamiliki wa vituo vya hali ya hewa nchini kuacha mara moja tabia ya kutoa taarifa zao kiholela kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi.

Dk. Chang’a,ametoa onyo hilo leo Mei 15,2023 jijini Dodoma wakati akifungua semina ya siku moja kwa ajili ya kujadili mapungufu yaliyopo katika mamlaka ya hiyo na kuyafanyia maboresho ili kufikia viwango vya kimataifa katika utoaji wa takwimu sahihi za hali ya hewa kwa maendeleo ya Taifa.

Dk. Chang’a amesema kuwa sheria namba 2 ya mwaka 2019 ya Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania inakataza mtu yeyote kusambaza taarifa na hali ya hewa bila ya kuwa na kibari.

“Sheria yetu inatoa maelekezo kwa mtu yeyote anaye sambaza taarifa kwa umma za hali ya hewa bila kuwa na kibali kwani kufanya hivyo unaweza kuzua taharuki kwa umma na ni kinyume na sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania namba 2 ya mwaka 2019”amefafanua Dk. Chang’a

Hata hivyo amewataka wananchi kuendelea kuzitumia taarifa zinazotolewa na vyanzo rasmi ikiwemo Mamalaka hiyo ya TMA, katika utekelezaji wa shunghuli zao za kila siku.

“Nitoe rai kwa wananchi kutumia taarifa zetu kutoka vyanzo rasmi ambazo zitawasaidia katika majukumu yao ya kila siyo na siyo katika vyanzo visivyo rasmi na ambavyo havijapatiwa kibari na serikali”ameeleza Dk. Chang’a

Kwa upande wake Alfrei Maseke, mwakilishi kutoka Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia maendeleo (UNDP), amesema kuwa semina hiyo inalenga kuiwezesha Tanzania katika kuboresha miundombinu ya hali ya hewa na kuongeza ufanisi wa taarifa zinazotolewa na TMA ili kuwa na tija katika jamii.

Sehemu ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa semina ya siku moja kwa ajili ya kujadili mapungufu yaliyopo katika Mamlaka ya hiyo na kuyafanyia maboresho ili kufikia viwango vya kimataifa katika utoaji wa takwimu sahihi za hali ya hewa kwa maendeleo ya Taifa leo Mei 15,2023 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’a akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya siku moja kwa ajili ya kujadili mapungufu yaliyopo katika Mamlaka ya hiyo na kuyafanyia maboresho ili kufikia viwango vya kimataifa katika utoaji wa takwimu sahihi za hali ya hewa kwa maendeleo ya Taifa leo Mei 15,2023 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang’akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina ya siku iliyofanyika leo Mei 15,2023 jijini Dodoma.
Alfei Maseke kutoka Mpango wa Umoja wa Mataifa Kusimamia Maendeleo Duniani (UNDP),akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina ya siku moja kwa ajili ya kujadili mapungufu yaliyopo katika Mamlaka ya hiyo na kuyafanyia maboresho ili kufikia viwango vya kimataifa katika utoaji wa takwimu sahihi za hali ya hewa kwa maendeleo ya Taifa leo Mei 15,2023 jijini Dodoma.