Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Kufuatia kuanza kwa mvua za msimu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imeitaka idara ya menejimenti ya maafa nchini kuendelea kuratibu utekelezaji wa mipango itakayosadia kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kipindi cha mvua
Akitoa taarifa hiyo kaimu mkurugenza Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Dk Ladislaus Chang’a, amezitaka malaka husika katika mikoa wilaya kata vijiji kutoa eklimu na mwongozo itakayohamasihsa kuzuia au kupunguza madhara
Hata hivyo wamezita sekta zinazotumia mamlaka ya hali ya hewa nchini kama wakulima, wafugaji mamlaka za wanyamapoli na wadau kuwasiliana na mamlaka ili kupata taarifa mahsusi za utabiri wa msimu ili kukidhi mahitaji katika sekta zao
Amesema mamlaka ya hali ya hewa inatoa taarifa ya uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za msimu kwa maneno yanayopata msimu mmoja wa mvua kwaka (kanda ya magharibikati,nyanda za juu kusii magharibi ,Kusini mwa nchi ukanda wa pwani ya kusini pamoja na maeneo yaliopo kusini mwa mkoa wa morogoro )
Amesema kuwa TMA inawatahadharisha wananchi uwepo wa mvua nyingi katika kipindi cha nusu ya kwanza ya msimu wa Novemba, 2023 hadi Januari, 2024 na kwamba zinaweza kusababisha mafuriko na kuathiri ukuaji wa mazao.
Imesema uwepo wa El-Niño unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mvua za msimu huo ikilinganishwa na kipindi cha nusu ya pili cha Februari hadi Aprili, mwaka 2024.
Chang’a ameyataja maeneo yatakayopata mvua za juu ya wastani kuwa ni Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, mikoa ya Iringa, Lindi, Mtwara, Singida, Dodoma, Kaskazini mwa Mkoa wa Katavi, Kigoma na Tabora.
Aidha, mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa Kusini mwa mkoa wa Katavi, mikoa ya Njombe, Rukwa, Songwe, Mbeya na Ruvuma.
Ameeleza kuwa mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Oktoba, 2023 katika maeneo ya Magharibi na kutawanyika katika maeneo mengine mwezi Novemba, 2023.
Dkt Chang’a amesema katika mvua hizo, athari zitakazojitokeza ni pamoja na vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo.
Vilevile amesema magonjwa kama vile ukungu yanatajariwa kuongezeka na kuathiri mazao kama viazi mviringo, nyanya, ufuta na maharage
Amefafanua kuwa msimu wa vuli kwa miezi ya Oktoba hadi Desemba, 2023 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka, mvua hizo zimeshaanza katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria, Pwani ya Kaskazini na baadhi ya maeneo ya nyanda za juu Kaskazini mashariki kama ilivyotabiriwa.
“Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani ikijumuisha kisiwa cha Mafia pamoja na Zanzibar (visiwa vya Unguja na Pemba) utabiri wake ulitolewa tarehe 24 Agosti, 2023,” amesisitiza.
Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika miezi ya Novemba na Disemba, 2023, vilevile, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika mwezi Januari na Februari, 2024.