Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa taarifa juu ya mwenendo wa uwepo hali ya El Niño katika bahari ya Pasifiki na athari zake nchini. 

Kwa Mujibu wa Taarifa ambayo imetolewa na Mamlaka hiyoleo imeeleza El Niño ni mfumo wa hali ya hewa unaosababishwa na uwepo wa ongezeko la joto la bahari la juu ya wastani katika eneo la kati la kitropiki la bahari ya Pasifiki.

Hali hio huambatana na athari mbalimbali ikiwemo ongezekola mvua, joto na hali ya ukame katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Aidha, ukubwa wa athari hizo unategemea nguvu pamoja na muda ambao hali ya El Niño itadumu, na pia inategemea hali na mwelekeo wa mifumo mingine ya hali ya hewa ikiwemomwelekeo wa upeopo na jotola bahari katika Bahari ya Hindi.Kwa Tanzania, hali ya hii ya El Niño huambatana na vipindi vya mvua kubwa na za juu ya wastani.

Mamlaka imeendelea kufuatilia mwenendowa mifumo ya hali ya hewa kiwemo El Niño. 

Kwa ujumla mifumo ya hali ya hewa inaonesha kuanza kujitokeza kwa El Niño,hali ambayo inatarajiwa kuimarika zaidi kuelekea mwishoni mwa mwaka 2023.Uchambuzi wa awali wa mifumo ya hali ya hewa unaonesha kuwa El Niño itakuwa na nguvu ya wastani.

Hata hivyo,athari za moja kwa moja hazijaanza kujitokeza katika maeneo ya nchi yetu kwa kipindi hiki cha kipupwe.

Aidha, Mamlaka imeendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo mbalimbali ya hali ya hewa kwa ukaribuna kufanya uchambuzi wa kina utakaoainisha athariza El Niño katika mifumo ya mvua hususanmsimu wa mvua za Vuli(Oktoba hadi Disemba),2023na taarifa hiyo itajumuisha ushauri stahiki kwa sekta mbalimbalina itatolewa kablaya kuanza kwa msimu.

Kwa upande mwingine, msimu wa Kipupwe(Juni-Agosti), 2023 bado unaendelea kama taarifa ya utabiri ilivyotolewa Mei, 2023.Vipindi vya upepo mkali pamoja na baridi vimeendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi. 

Hali ya baridi kali imeendelea kujitokeza katika maeneo ya nyanda za juu kusini magharibi(ikijumuisha mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa)na maeneo ya miinuko ya nyanda za juu kaskazini mashariki. Katika kipindi cha mwezi Julai, 2023 kiwango kidogo zaidi cha joto la chini cha nyuzi joto 2.50C kimeripotiwa katika kituo cha Uyole, Mbeya mnamo Julai 5 2023.

Kwa taarifa hii wananchi wanashauriwa kuendelea kuzingatia taarifa na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania sambamba na kutafuta, kupata na kuzingatia ushauri wa wataalam katika sekta husika ili kupunguza athari zinazotokana na hali mbaya ya hewa.

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa kwa ujumla na kutoa mrejeo kila itakapobidi.

Please follow and like us:
Pin Share