Mahakama ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa katika mikoa nane itakayonyesha kwa siku tatu kuanzia kesho Aprili 29 hadi Mei Mosi 2023.

Taarifa iliyotolewa na TMA leo Aprili 28, 2023 angalizo hilo la mvua kubwa limetolewa katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Tanga, Lindi, Mtwara, visiwa vya Unguja na Pemba, Mara, Simiyu na Mwanza.

Aidha mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuanzia Aprili 29, 2023 katika baadhi  ya maeneo ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia)Tanga, Lindi, Mtwara pamoja ma visiwa vya Unguja na Pemba, huku katika mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu mvua hizo zinatarajiwa kunyesha Aprili 30 na Mei Mosi, 2023.

Athari zinazoweza kujitokeza katika kipindi hicho ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji hali inayoweza kuchelewesha baadhi ya shughuli za uchumi na usafirishaji.

Mamlaka inawashauri watu wote kuendelea kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa mara kwa mara.
 

HABARI