Mwwnyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Buruhani Nyenzi amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Kanda ya Mashariki na Kituo cha kutoa tahadhari za TSUNAMI nchini, unaotekelezwa katika maeneo ya SIMU 2,000, Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mradi huo ambao utagharimu zaidi ya shilingibl bilioni 9 za kitanzania, unatarajiwa kukamilika mwezi Julai,2024.
Akizungumza wakati wa ziara yake, Dk. Nyenzi amesema, chini ya Serikali ya Awamu wa Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, mamlaka imekuwa wanufaika wakubwa katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini ukiwemo mradi huo ambao utahusika moja kwa moja katika utoaji wa tahadhari za TSUNAMI nchini na hivyo kuongeza tija katika mipango ya nchi.
Aidha, Dkt. Nyenzi alifurahishwa na kasi ya ujenzi unavyoendelea kutokana na hatua mbalimbali ambazo mkandarasi amezichukua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi muda wa ziada na kuongeza nguvu kazi ili kuhakikisha makubaliano ya kimkataba yaliyowekwa yanafikiwa kwa wakati.
Dk. Nyenzi alisisitiza matumizi ya malighafi zenye ubora na kutoa fursa za ajira kwa wazawa katika mradi huo.