Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia kesho Novemba 11 katika maeneo mbalimbali nchini.
TMA imesema mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha kwa muda wa siku tatu kwenye mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga, Tabora, Kigoma na Katavi.
Kutokana na mvua hizo wananchi na wadau wa hali ya hewa wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na athari zinazoweza kujitokeza ikiwemo mafuriko katika baadhi ya maeneo, madaraja kuzingirwa na maji na shughuli za usafiri kukwama.