Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Taasisi ya Tanzania Islamic Studies Teaching Association wameipongeza Serikali na wadau kwa kuboresha mitahala ya masomo ya dini ya kiislamu na kuongeza ufaulu.

Akizungumza kwa kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti Shekh Ku’ndecha amesema  kama taasisi wamelizishwa na mchango mkubwa wa Serikali na wadau wote walishiriki kufanikisha mtaala wa masomo ya dini ya Kislamu katika mashule unaboreshwa

“Tunaishukuru  Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa maboresho ya mitaala iliyopelekea ufauru mzuri wa somo la dini

“mbapo kupitia hatua hiyo zimeanzishwa taasisi mpya zinazo husisha masomo ya dini katika ngazi ya sekondari ya juu kidato cha tano na sita pamoja na kutoa kibali cha kubadili lugha ya kufundishia somo la
elimu ya dini ya kislamu kidato cha tano na sita kutoka lugha ya kiingereza kuwa lugha ya kiswahili kuanzia mwaka 2025.

“Matarajio yetu makubwa kuanzia 2025 serikali itaanza kudahili somo la elimu ya dini ya kiislamu, katika  shule za msingi kupitia Baraza la Mitihani  kama inavyofanyika sasa kuanzia ngaizi ya sekondfari na vyuo
vya ualimu.

Aidha tista inawapongeza watahiniwa wote waliofanya mitihani ,kwa kuwa na utulivu na kuzingatioa taratibu zinazotakiwa  kwa kipindi chote cha uendeshaaji wa mitihani mpaka kupata matokea mazuri”amesema

Kundecha amesema matokeo ya mitihani wa kuhitimu elimu ya msingi kwenye somo la elimu ya dini ya kislamu lugha ya kiaramu na madrasa ulifanyika  mwezi Agosti 2024 imeonyesha kuongezeka kwa ushiriki
kwenye halmashauri kutoka 159 mwaka 2023 hadi 162.

Idadi ya shule zilizofanya mitihani zimeongezeka kutoka 3,975 mwaka
2023 hadi 4,583 mwaka huu, pia idadi ya watainiwa imeongezeka kutoka 167,823 mwaka 2023 hadi 163,430 mwaka 2024 sawa na asilimia 3.6.

Mwaka huu jumla shule 4583 kutoka katika halmshauri 162 kwenye mikoa 28 ya Tanzania bara na Visiwani, zilizosajiliwa  ambapo  watainiwa  wa somo la elimu ya dini ya kislamu walikuwa 178,803 .

Kati yao Wasichana 96, 535 sawa na asilimi 54 na Wavulana 82,268 sawa na asilimi 46,wenye mahitaji maalumu walikuwa 7 sawa na asililimi 0.004 ya watainiwa wote.

Watahiniwa waliofanya mithani 163,430 sawa na asilimia 91.4 ya wanafunzi waliosajiliwa, ambapo Wasichana ni 89,887 sawa na asilimi 55 na wavulana ni 73,543 sawa na asilimi 45, wenye mahitaji maalumu walikuwa 7 sawa na asilimi 100

Watainiwa ambao hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ni
15 ,373 sawa asilimia 8.6

Matokea ya somo la kiarabu jumla ya shule 29  kutoka katkika mikoa kumi ya Tanzania bara na Visiwani, zilisajiliwa kufanya mitihani jumla ya watainiwa  wa somo la lugha ya kiarabu walikuwa 1,080  ambapo wasichana walikuwa 569  sawa na asilimi 52.7 na Wavulana 511 sawa  na asilimia 47 .3 ya watainiwa wote.

Watainiwa waliofanya mtihani 1069  ambapo Wasichana 564 sawa na asilimia 52 .8 na wavulana 505 sawa na asilimi 47.2 ya watainiwa wote watainiwa ambo hawakufanya mtihani kutokana na sabau mbalimbali 11 sawa na asilimia 1.0.

Idadi ya shule zilizofanya mtihani zimeongezeka kutoka 24 mwaka 2023
hadi 29  mwaka huu ambapo swa  na ongezeko la asilimia 20.8 hali kadhalika ,idadi ya watainiwa imeongezeka kutoka 697  mwaka 2023 hadi 1,069 sawa na ongezeko la asilimia 53.4

Mtihani ulikuwa  na jumla ya alama hamsini  mtahiniwa amehesabiwa kuwa
amefauru, ikiwa amepata daraja A ,B au D ambapo kwa sasa ufauru umeongezeka kwa asilimia 0.5 kutoka asilimia 96.7 ya watainiwa walio faulu kwa kupata daraja A hadi D mwaka 2023 hadi asilimia 97.2 mwaka
2024 idadi ya watainiwa wote.

Matoke ya mtihani wa madrasa kulikuwa na jumla ya wataini 217 waliofanya mtihani 187 sawa na asilimi 86.18 ,idadi ya watainiwa ambao hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali ni 30 sawa na asiimia 13.82

Idadi ya mikoa iliyoshiriki imeongezeka kwa asilimia 71.43 kutoka mikoa 7 mwaka 2023 hadi mikoa 12 mwaka 2024 idadi ya madrasa nayo imeongezeka kwa asilimia 61.5 kutoka madrasa 13 mwaka 2023 hadi
madrasa 21 mwaka 2024.

Please follow and like us:
Pin Share