Michuano ya Kombe la Mapinduzi, inafungua pazia leo visiwani Zanzibar, ambapo Kilimanjaro Stars kutoka Tanzania bara itakutana na timu ya taifa ya Zanzibar Heroes usiku wa leo, katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.

Timu nyingine zitakazoshiriki michuano hiyo ni Burkina Faso kutokea Afrika Magharibi na Harambe Stars kutoka Kenya, ambao watacheza kesho katika uwanja huo huo.

Timu ya taifa ya Burundi na Uganda The Cranes zilijitoa katika mashindano hayo dakika za mwisho na kuifanya michuano hiyo kubaki na timu nne pekee.

Kombo la Mapinduzi hufanyika kama sehemu ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar yaliyotokea Januari 12 mwaka 1964, yaliyoondoa utawala w Kisultani katika visiwa hivyo ambavyo kwa sasa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.