Na Lookman Miraji,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Timu ya taifa ya mchezo wa tenis imesafiri asubuhi ya leo hii kuelekea nchini bostwana kushiriki mashindano ya Dunia kanda ya tano kwa ukanda wa Afrika.

Akizungumza hapo jana katika hafla ya kuagwa kwa timu hiyo Afisa wa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Ndg; Charles Maguzu ameipongeza kamati tendaji ya chama cha mchezo tenis nchini kwa maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa kuiandaa timu hiyo pamoja na kutoa pongezi kwa benchi la ufundi wa timu hiyo likiongozwa na kocha mkuu kuhakikisha kuwa wamepata wachezaji ambao wanaubora unaotakiwa kwaajili ya kuliwakilisha taifa.

Afisa Maguzu amesema ya kuwa wanawaaga wachezaji hao wakiwa wanajua kuwa wanauzoefu wa kutosha kupitia mashindano yaliyopita , hivyo wanategemea kuona timu hiyo ikishika nafasi za juu zitakazopelekea timu hiyo kufuzu kushiriki mashindano ya juu zaidi.
Mbali na hayo Maguzu amewasihi wachezaji hao kujenga urafiki wa karibu na wachezaji wengine ili kurithishana ujuzi na wachezaji wengine.

Kwa upande wa nahodha wa kikosi hicho Hamisi Omary ameishukuru serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa BMT katika jitihada zao za kusapoti Michezo. Nahodha Hamisi pia ameongeza kwa kuwaahidi watanzania kutarajia mazuri kwani kama wachezaji wako tayari kupambana kwaajili ya taifa.

Kwa upande wa kocha mkuu wa timu hiyo Ndg; Salum Mvita naye amesema ya kuwa yuko na kikosi hicho karibuni mwaka wa tatu sasa, kwahiyo timu imeandaliwa vizuri sana na kila mwaka ndivyo ari ya wachezaji kufanya vizuri inaongezeka.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kufanyika mnamo tarehe 15 mpaka tarehe 20 ya mwezi huu julai nchini Bostwana.

Please follow and like us:
Pin Share