Jakarta, Indonesia
Watu zaidi ya 380 wamethibitishwa kufa
baada ya tsunami kusababisha tetemeko la
ardhi lenye ukubwa wa Richter 7.5, lililopiga
mji wa Jakarta mwishoni mwa wiki.
Upepo mkali ulivuma kutoka Palu katika
Kisiwa cha Sulewesi kwa mita tatu. Video
inayoonekana kwenye mitandao ya kijamii
inaonyesha jinsi watu walivyokuwa wakipiga
kelele huku wakikimbia kwa hofu.
Baada ya mshtuko wa tetemeko hilo, maelfu
walizimia majumbani mwao huku wengine
wakielekea hospitalini, hotelini na kwenye
maduka makubwa.
Jitihada za uokoaji zinaendelea ingawa
zimepata changamoto ya umeme kukatika.
Njia kuu ya Palu imefungwa kutokana na
daraja kuu kuvunjika.
Miili mingi imepatikana ufukweni
Mamlaka ya maafa nchini Indonesia
inasema watu 384 wamekufa ingawa idadi
inategemewa kuongezeka na watu 540
wamejeruhiwa.
Miili mingi ilikutwa ufukweni kwa sababu ya
tsunami, lakini idadi yake bado
haijafahamika.
Msemaji wa Serikali, Sutopo Purwo
Nugroho, ameliambia Shirika la Habari la
Reuters kuwa wakati onyo lilipotolewa, watu
waliendelea na shughuli zao ufukweni na
hawakuchukua tahadhari ya kukimbia mara
moja, hivyo wakawa miongoni mwa
wahanga.
Wengine waliokoka kwa kupanda miti ili
kukimbia upepo mkali.
Tetemeko hili lilianza kwa kutangulia kwa
tetemeko jingine dogo lililoua mtu mmoja na
wengine 10 kujeruhiwa, wakiwa katika soko
dogo la samaki huko Donggala.
Mjini Palu mamia ya watu walikuwa
wanajiandaa kwa ajili ya tamasha lililokuwa
linatarajiwa kuanza Ijumaa jioni.
hospitali kuu imeharibiwa na tetemeko la
ardhi, hivyo watu wengi imewabidi kupata
huduma wakiwa nje.
Palu na Donggala ni miji yenye makazi ya
watu zaidi ya 600,000. Rais wa nchi hiyo,
Joko Widodo, amesema makundi ya
waokoaji yanaendelea kuelekea katika
sehemu iliyopata janga ili kutoa msaada
zaidi.
Uwanja wa Ndege wa Palu umefungwa
kutokana na tsunami ingawa helikopta
zitaendelea kufanya kazi. Jeshi la nchi hiyo
litatuma ndege za jeshi kutoka mji mkuu wa
Jakarta.
Mamlaka ya hali ya hewa ya Indonesia
inalaumiwa kwa kuchelewa kutoa angalizo
kwa sababu onyo kuhusu tsunami lilitolewa
ndani ya saa moja kabla ya tsunami kupiga.
Inakumbukwa kuwa mwaka 2004 tsunami
ilisababisha tetemeko la ardhi nchini
Indonesia na watu zaidi ya laki mbili
walifariki dunia.
Mwaka 2010 pia zaidi ya watu 282
waliuawa kutokana na tsunami
iliyosababishwa na tetemeko la ardhi katika
pwani ya Sumatra nchini Indonesia.
Mwisho