Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma

MAMLA ya Elimu Tanzania (TEA), kupitia mradi wa Mfuko wa kuendeleza ujuzi imefanikiwa kuwafikia vijana 49,063 kupitia mafunzo katika sekta za kilimo,uchumi, TEHAMA , Utalii, nishati,ujenzi na uchukuzi.

Imesema vijana walionufaika ni pamoja na vijana 464 wanaotoka kundi la wenye ulemavu, vijana 2,928 waliotoka kundi la vijana kutoka katika kaya maskini ma wanaoishi katika mazingira magumu.

Hayo yalibainishwa jijini hapa Leo Agosti 10,2023 Jijini hapa na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bahati Geuzye wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.

“Utekelezaji wa miradi chini ya mfuko wa kuendeleza ujuzi (SDF) katika awamu ya kwanza umekamilika ambapo serikali imefanikiwa kufikia lengo la utekelezaji kwa kiwango cha juu.Kupitia miradi hiyo TEA imefanikiwa kufikia wanufaika 49,063 sawa na asilimia 114 ya wanufaika waliolengwa.”

Amesema kati ya wanufaika hao wanawake ni 22,413 sawa na asilimia 46 na wanaume 26,650 sawa na asilimia 54 ya wanufaika wote.Vijana walionufaika ni pamoja na vijana 464 waliotoka kundi la wenye ulemavu, vijana 2,928 waliotoka kundi la vijana utoka katika kaya maskini ma wanaoishi katika mazingira magumu.”

Bahati amefafanua kuwa ufuatiliaji wa mafunzo hayo ulifuatiliwa na kuonyesha kuwa asilimia 80 ya wanufaika wameweza kujiajiri au kuajiriwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa katika mwaka huu wa fedha TEA imepanga kutumia sh.bilioni nane kwa ajili ya kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

Amefafanua kuwa fedha hizo zitatumika kufadhili miradi 82 katika shule 81 zikiwemo shule 48 za msingi na 33 za sekondari katika maeneo ya Tanzania bara.

“Miradi hii itakapokamilika itanufaisha wanafunzi 39,484 na walimu 169 katika shule za msingi na sekondari.Miradi itakayofadhiliwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 82, matundu ya vyoo 336, mabweni10, ujenzi wa maabara 18 za masomo ya sayansi na nyumba za walimu 32,”ameeleza.

Ameongeza kuwa ;”Katika mwaka huu wa fedha TEA itatoa ufadhili kwa ajili ya uboreshaji wa miundombunu kwa kuwezesha ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika taasisi moja ya elimu ya juu,”amesema

Kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka uliopita, Bahati amesema, TEA imetumia sh.bilioni 10.9 kugharamia ufadhili wa miradi 132 ya kuboresha elimu ikiwemo ujenzi wa madarasa, maabala na matundu ya vyoo katika shule 151 nchini

Please follow and like us:
Pin Share