Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt.Jabiri Bakari,amezitaja changamoto katika sekta hiyo nchini kuwa ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ya mawasiliano.
Hayo ameyasema leo Novemba 3,2022 jijini Dodoma,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
“TCRA imendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwenye kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kulinda miundombinu ya mawasiliano”amesema Dkt.Bakari
Amesema, changamoto nyingine ni utoaji wa huduma za mawasilino kwa wote kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa bado.
Hata hivyo, amebainisha namna ambavyo wamekuwa wakikabiliana na kero hizo kupitia kituo cha kitaifa cha usalama mtandaoni (TZ-CERT) kimeendelea kukabiliana na uhalifu mtandaoni ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wadau.
“TCRA imendelea kusimamia ubora wa huduma za mawasilinao kwa kutumia mitandao ya kisasa ili kuhakikisha huduma zinazaotolewa na watoa huduma zinakidhi viwango bora”amesema
Amesema kuwa TCRA inaendelea kuboresha na kusimamia kanuni za mawasiliano ya Kielectroniki na postal (Online Contents) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Jeshi la Polisi,BASATA pamoja na Mahakama