Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia, Dodoma.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)kupitia Mfumo wake wa Usimamizi wa simu za ndani na kimataifa imebaini idadi ya dakika za simu za kimataifa zinazoingia nchini kupungua kutoka dakika 3,136,692 mwezi Julai 2022 hadi kufikia 2,900,165 mwezi Juni 2023 sawa na asilimia 7.54.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk.Jabir K Bakari ameeleza hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa Mamlaka hiyo jijini Dodoma na kueleza kuwa idadi ya dakika za simu za kimataifa zinazotoka nchini zimepungua kutoka dakika 2,405,522mwezi Julai 2022 hadi kufkia dakika 2,226,071 mwezi Juni 2023 sawa na asilimia 7.46.
Amefafanua kuwa kupungua kwa simu za kimataifa kunasababishwa na mabadiliko ya teknolojia na upatikanaji wa chaguzi mbadala za kupiga simu kupitia
mitandao ya intaneti kama vile Whatsap, Facebook, Telegram, Zoom nakadhalika.
“Idadi ya dakika za simu za kitaifa ndani ya mtandao mmoja (onnet) zimeongezekakutoka dakika 6,172,696,579 mwezi Julai 2022 hadi dakika 7,012,574,045 mwezi Juni 2023ambayo ni sawa na13.61% hivyo hivyo idadi ya dakika za simu za kitaifa nje ya mtandao mmoja (offnet)
zimeongezeka kutoka dakika4,879,102,325 mwezi Julai 2022 hadi kufikia dakika 5,064,800,480 kufikia mwezi Juni 2023 ambayo nisawa na 3.81%,”amesema
Amesema ongezeko la simu za kitaifa linasababishwa na ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchini na kwamba katika Kubaini simu za ulaghai TCRA imeendelea kubaini simu za ulaghai zinazoingia hapa nchini na hatua stahiki zimekuwa zikichukuliwa.
” Kutokana na hatua hiyo, idadi ya simu za udanganyifu imeendelea kupunguakuanzia mwaka 2020 hadi Juni 2023, tulibaini matukio machache ya simu za ulaghai yalitokea ,katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 mpaka Juni 2023, TCRA imeendelea kuwasimamia watoa huduma za mawasiliano kwa kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa masharti ya leseni zao pamoja na kuzingatia viwango vya ubora ,”amesma.
Dk.Bakari pia alisema, TCRA imefanya maboresho makubwa ya mifumo ya udhibiti wa Sekta ambapo kwa sasa wamejenga uwezo wakufuatilia ubora wa huduma tukiwa ofisini, ili kuhahikisha watoa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti, utangazaji (Radio na Televisheni) na posta wanatoa huduma kwa ufanisi na kwa kuzingatia ubora.
“Aidha, TCRA ilifanya ufuatiliaji na kuhakikisha utekelezaji wa masharti ya kanuni na sheria katika maeneo ya ukaguzi wa watoa huduma kwa kukaguzi watoa huduma 671
wa simu na intaneti, utangazaji na postaili kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa sheria, kanuni, miongozo na masharti ya leseni,”alifafanua
Alisema TCRA ilitoa maelekezo, onyo, na adhabu kwa watoa huduma waliokutwa na ukiukwaji wa sheria, kanuni, miongozo na masharti ya leseni ikiwa ni pamoja na Upimaji wa Ubora wa hudumaza mitandao ya simu katika mikoa ishirini na nne (24), Tanzania Barana mikoa yote yaZanzibar na kukutana na watoa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti kila robo mwaka kujadili
matokeo ya upimaji wa ubora wa mitandao ya simu.
“Upimaji wa hivi karibuni ulifanyika kuanzia mweziAprili hadi Juni, 2023 umehusishamakampuni (06) ya simu katika maeneo ya miji saba (07) ambayo ni Kahama, Songwe, Mbeya, Kigoma, Katavi, Tabora, and Rukwa.
Taarifa za matokeo yaupimaji wa ubora wa huduma za mawasiliano na maendeleo ya sekta zinapatikana kupitia viunganisho vya https://t.ly/nLrwI(Taarifa ya Maendeleo ya Sekta Aprili-Juni 2023) 2.https://t.ly/Hpob6(Matokeo ya Upimaji wa Ubora wa Mawasiliano ya simu Aprili -Juni2023),”alifafanua
Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo wa TCRA alibainisha kuwa katika ukaguzi wa masafa,TCRA hutekeleza ukaguzi huo kila robo mwaka kujua kiwango cha matumizi ya masafa iliyoyagawa kwa watoa huduma nchi nzima na kuhakikisha hakuna muingiliano wa masafa.
Alisema TCRA imeendelea kutatua changamoto za muingilianowa masafa zilizoletwa na watoahuduma na
zilizoonekana wakati wa upimaji kama vile muingiliano wa masafa yanayotumika kwa huduma za mawasiliano ya ndege ili kuhakikisha usalama kwa huduma hiyo, muingiliano katika masafa ya radio ili kuhakikisha ubora wa usikivu na muingiliano wa masafa ya simu ili kuboresha huduma za simu.