Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia Dar es Salaam

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) wanatarajia kuendesha Operesheni ya kuwaondoa wadaiwa sugu 648 katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Mara Oktoba 7, 2024.

Pia imeelezwa kwamba licha ya kuondolewa wadaiwa hao katika nyumba za wakala hao, hatua nyingine itakayofuata kwa atakayeshindwa kulipa deni atafikishwa mahakani.

Akizungumza leo Oktoba 2, 2024 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Majengo TBA, Daud Kondoro amesema hayo hatua hiyo ya kuwaondoa wadaiwa sugu imekuja baada ya kuwapa notisi ya siku saba.

Ameongeza kuwa wadaiwa sugu wanaotarajiwa kuondoshwa ni 648 ambao tayari wamepewa notisi ya wiki mbili ili kufanikisha mchakato wa kulipa malimbikizo ya madeni iliyofikia Shilingi bil 14.8/-.

Ameongeza kuwa katika mikoa hiyo minne deni ambao wateja wanadaiwa ni bilioni 1.7 na tunawataka kuhakikisha wanalipa kwa wakati mara baada ya kupokea ujumbe mfupi wa kumbukumbu ya malipo ambayo utumwa kwao kila mwezi.9.

“Kwa kweli changamoto ya madeni kwa wapangaji imekuwa ni sugu na hatua kadhaa zimekuwa zikichukukuwa kudhibiti hilo, moja ni kuwaondoa katika nyumba na kabla ya kuwafikisha mahakamani huwa tunazungumza nao namna watakavyoweza kulipa,” anasema.

Ameongeza kuwa jukumu la kuwaondoa wadaiwa hao sugu wamekabidhiwa dalali wa Mahakama, Twins Action Mart na wapo tayari kutekeleza jambo hilo.

Ameongeza ili kukabiliana na mchakato wa kukusanya madeni hususan kwa watumishi wa Serikali wamewekewa mfumo wa kieletroniki wa Usimamizi wa Miliki za Serikali (GRMS) utakaosaidia kuboresha ukusanyaji wa kodi.

Mfumo huo utawawezesha watumishi wa umma, kulipa kodi moja kwa moja kutoka kwenye mishahara yao.

Mkurugenzi Kondoro amefafanua kuwa kwa sasa wanaendelea na mchakato wa kufunga vitasa janja na smart meter katika nyumba hizo kwa lengo kuimalisha ukusanyaji madeni kwa wadaiwa sugu

Pia wapangaji na wadaiwa sugu, wamesisitizwa kufuatilia taarifa zao kupitia mtandao rasmi wa kijamii wa TBA na si vinginevyo.