Mabunge mawili ya Bunge la Ethiopia yamemchagua Taye Atske Selassie, Mwanadiplomasia kuwa Rais wa nchi hiyo.

Taye Atske Selassie ameapishwa Oktoba 07, 2024 na kukabidhiwa katiba na Rais wa nchi anayemaliza muda wake.

Taye anachukua mikoba ya Rais wa kwanza Mwanamke wa nchi hiyo ambaye alichaguliwa miaka sita iliyopita katika wadhifa ambao Mamlaka ya Utendaji yakiwa chini ya Waziri Mkuu.

Taye ni Mwanadiplomasia mwenye uzoefu, aliwahi kuwa Balozi wa kudumu wa Ethiopia katika Umoja wa Mataifa huko New York.

Zewde, ambaye ameweka historia ya kuwa Rais wa kwanza Mwanamke wa Ethiopia mwaka 2018, alijiuzulu kama mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika ili kushika wadhifa wa Rais wa Jamhuri ya Ethiopia.

Kulikuwa na ripoti za mtafaruku kati yake na Waziri Mkuu Abiy Ahmed.