Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Lawrence Tax, Mkuu wa Mjeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda, Wambata Jeshi wa Jeshi Rafiki pamoja na Mabalozi wakishuudia Vikundi vya Makomando Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika zoezi la kulenga Shabaha ( Mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China ) yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Uwanja wa Mashabaha, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mkuu wa Mjeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda akizungumza jambo wakati wa kufunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Msaidizi Mkuu wa Majeshi, Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Meja Jenerali Ye Dabin akizungumza jambo wakati wa kufunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Askari wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China wakiwa katika picha ya pamoja katika zoezi la kufunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika picha ya pamoja katika zoezi la kufunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mkuu wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona akizungumza jambo wakati wa kufunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Lawrence Tax akigawa vyeti kwa Askari wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China wakati akifunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Msaidizi Mkuu wa Majeshi, Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Meja Jenerali Ye Dabin akigawa vyeti kwa Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakati wa kufunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
Picha za matukio mbalimbali katika zoezi la kufunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani. Askari wa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China wakiwa katika picha ya pamoja katika zoezi la kufunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani.
…………….
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Lawrence Tax amefunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ pamoja ushirikiano na China yaliofanyika katika Kambi ya CTC Mapinga, Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Katika zoezi hilo la kufunga Mazoezi ya Medani, Umoja 2024 viongozi mbalimbali wa Jeshi wakiwemo wambata Jeshi wa Jeshi Rafiki, Mabalozi wameshuudia matukio mbalimbali ya kijeshi yaliofanywa na JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China ikiwemo namna ya kuzuia ugaidi, kuokoa watu mashuhuri pamoja zoezi shabaha kwa kutumia silaha ndogo za kivita.
Akizunguma wakati akifunga mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China yaliofanyika Agosti 11, 2024 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Tax, amesema kuwa kupitia mazoezi ya pamoja yaliofanywa majini na Nchi kavu wamepata faida ya kuimarisha uwezo wa Jeshi la JWTZ, kudumisha undugu pamoja na kuendeleza umoja.
Mhe. Tax amesema kuwa Tanzania na China wamekuwa na marafiki kwa muda mrefu, hivyo mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 yameimarisha ushirikiano katika kuhakikisha wanaendelea kufanya kazi kwa ufanisi.
“Mnapofanya kazi pamoja inasaidia kubadilishana uzoefu na hivi sasa dunia inakwenda katika Teknolojia na ukiangalia matishio ya uvunjifu wa amani yamebadilika, hivyo unavyoshirikiana mnaweza kupashana habari” amesema Mhe. Tax.
Mhe. Tax amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suruhu Hassani kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na mataifa mbalimbali ikiwemo China ambapo kwa sasa umeimarika kwa kuruhusu kufanya mazoezi ya pamoja ya Medani, Umoja 2024 kati JWTZ pamoja na Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China.
Mkuu wa Mjeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda, amesema kuwa kupitia mazoezi ya Medani, Umoja 2024 wameweza kufanya tathmini ya Jeshi ili kujua lina uwezo kiasi gani.
“Tumeona uwezo wa Jeshi letu, Jinsi vijana walivyokuwa na morali wa hali ya juu na jinsi walivyofanya vizuri katika mazoezi ya shabaha, pia yamesaidia kuongeza hamasa kwa askali wetu kwani hawajafanya mazoezi ya pamoja na wezao kutoka Nchi mbalimbali dunaini ikiwemo China” amesema Jenerali Jacob Mkunda.
Jenerali Jacob Mkunda amemshukuru Rais Dkt. Samia Suruhu Hassani kwa kuliwezesha Jeshi kupata vifaa vya kisasa ambavyo vinawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kijeshi kwa ufanisi.
Mazoezi ya medani, Umoja 2024 yamefanyika kwa muda wa siku 14 katika Kambi ya CTC Mapinga, Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo JWTZ pamoja na Jeshi la Ukombozi wa Watu wa China walishiriki mazoezi ya pamoja.