📍Katika kuadhimisha Kilele cha Siku ya Kimataifa ya wanawake Machi 08, 2025, wanawake shupavu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA pia walikuwepo katika mji wa Ifakara, Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro kuungana na maelfu ya wanawake wengine kutoka mashirika, taasisi mbalimbali na wanawake wakazi wa Mkoa huo Kwa ujumla wake kuadhimisha siku hiyo yenye kauli mbiu “Wasichana na Wanawake 2025, Tuimarishe Usawa, Haki na Uwezeshaji”.

Wanawake wahifadhi wa TAWA wamekuwa mstari wa mbele katika kuadhimisha Siku hiyo adhimu katika mikoa mbalimbali nchini na kutumia fursa hiyo kuuonesha umma wa watanzania namna taasisi hiyo inavyotekeleza Kwa vitendo kauli mbiu ya mwaka 2025.