Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea
Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Shadrack Mziray ameagiza viongozi wa Halmashauri ambazo zinatekeleza miradi mbalimbali ya TASAF ikiwemo ujenzi wa zahanati, stendi pamoja na nyumba za wauguzi kusimamia miradi hiyo ili ifanyike kwa usanifu.
Agizo hilo amelitoa Oktoba 3,2024 wakati wa ziara yake mkoani Ruvuma ya kukagua miradi inayotekelezwa na TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua miradi inayoendele kutekelezwa ambapo miradi iliyokaguliwa ni stendi kuu ya Halmashauri ya Lundusi,ujenzi wa nyumba mbili za watumishi wa Afya,Maji katika zahanati ya Mdundualo na stendi ya kijiji cha Parangu
Amesema,TASAF inahudumia walengwa 1.3 milioni wanaowahidumia wamefanya tathimini na kujilidhisha kuwa walengwa 394 hali zao za maisha yao yamebadilika hivyo wamewaondoa kwenye alipo kwani wanajiweza pia wamefika kuangalia kama Kuna malalamiko ya wananchi nawamebaini hakuna.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo mratibu wa TASAF Halmashauri ya wilaya Songea Hosana Nguruge amesema wanaishukuru serikali kwa kuwapelekea miradi na miundombinu wamepata standi mbili ambapo standi ya Lundusi wamepokea sh.600 milioni ambayo inaendelea kutekelezwa na standi ya parangu wamepokea zaidi ya sh 300milioni na itakamilika mwezi Novemba 2024.
Amesema, nyumba za wauguzi wamepokea sh 154 milioni na kujenga kisima kirefu na matundu sita ya vyoo pamoja na Zahanati mdundualo hivyo kusogeza huduma za matibabu karibu na maeneo wanayoishi.
Naye Modestus Bishonga Mkazi wa kijiji cha Mdundualo amepongeza miradi hiyo ya TASAF kwani ulibuliwa na wananchi wenyewe na wanausimamia hivyo ameomba washirikiane kukamilisha miradi kwa wakati kwani imesaidia kuondoa kero kwa wananchi na kubadilisha hali zao za maisha na kwamba hakuna mwanaanchi anayelalamika.
“Miradi hii ya ujenzi wa stendi na zahanati tuliibua wananchi wenyewe na tunaisimamia umetuindolea kero wanachi ya kupata huduma bora za afya katika maeneo yetu tunayoishi pia uwepo wa nyumba za wauguzi umesaidia sisi kupata huduma kwa haraka kwani wauguzi wanaishi kqenye maeneo yetu tunaipongeza sana TASAF kupitia serikali kwa ubunifu huu wa miradi ya jamii,”
Naye sanasa William muuguzi wa Afya zahanati ya amesema wanaishukuru serikali na TASAF kwa kujenga nyumba za wauguzi kwani awali walikuwa wakiishi mbali na zahanati hiyo hivyo wananchi walipata adha kuwatafuta hasa kipindi cha usiku na maska.
Amesema kwa siku wanahudumia watu 30 au zaidi lakini kipindi cha chanjo wanahudumia watu wengi zaidi