Na Cresensia Kapinga,JamhuriMedia,Songea
JUMLA ya sh.milioni 389.8 zimetolewa na wakala wa barabara za mijini na vijijini(TARURA),Manispaa ya Songea,kujenga ujenzi wa boksi karavati na barabara ya rami kwa kiwango chepesi 0.71cm yenye urefu wa mita 700 ikiwa ni mwendelezo wa ujenzi wa barabara ya Tunduru JCT -Seedfarm yenye lengo ya kuwaondolea adha wananchi ya vumbi kujaa kwenye nyumba zao,matope na mifereji kuziba msimu wa mvua.
Akizungumza na JAMHURI,jana Kaimu Meneja Wakala wa Barabara za mijini na Vijijini (TARURA), Wilaya ya Songea,Mhandisi Johson Kweka amesema mradi huo unajengwa na mkandarasi M/S OVANS Construction LTD Mbinga,Kwa gharama ya sh.389,834,800 ulianza rasmi Agosti 18, mwaka huu, na unatarajia kukamilika Desemba 16, mwaka huu.
Amefafanua kuwa mradi huo utawanufaisha wakazi wa kata ya Seedfarm,Bombambili,Msamala,Mshangano pamoja na Mletele ambapo tayari kazi imeshafanyika kwa asilimia 60 ambapo boksikaravati limeshakamilika bado kujaza udongo
Naye Mhandisi Davis Mbawala amesema kwa sasa kazi inayoendelea ni kuhamisha miundombinu ya maji pamoja na umeme ndipo waaanze kutengeneza barabara kwa kiwango cha rami na kazi inaendelea vizuri
Aidha ametoa ushauri kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kutunza miundo mbinu ya barabara kwani barabara hizo ni zao .
Naye mkazi wa Seedfarm Lazaro Bunungu ameishukuru Serikali kwa kuweza kujenga barabara hiyo kwani itawasaidia kupunguza adha ya vumbi kwenye nyumba zao,matope kipindi cha mvua, pamoja na mifereji kuziba kipindi cha mvua hali ambayo ilisababisha barabara hiyo kushindwa kupitika ,ikiwa ni pamoja kupeleka miradi mingine ya barabara kwenye maeneo hayo ili kuondoa adha kwa wananchi
“Mradi huu wa ujenzi wa barabara mita 700 ni msada mkubwa kwetu ,kabla ya ujenzi huu tulikuwa tunapata shida kutoka barabara kubwa hadi kuingia bara bara ya mtaa huu,kulikuwa na utelezi mkubwa, na miteremko kutokana na maji kujaa barabarani, pia tulikuwa na daraja la miti hivyo magari makubwa yalikuwa yanashindwa kupita.
“Naamini mradi huu utasaidia sana kutunufaisha wananchi wote wa manispaa,utasaidia sana kuunganisha kata mbali mbali za Manispaa ya songea na utaondoa kero ya muda mrefu ya vumbi ,na matope kwenye makazi yetu hivyo kuweza kurahisisha upatikanaji wa huduma mbali mbali kwa nyakati zote ,”amesema Bunungu.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kulinda miundombinu ya Barabara hiyo kwani wao ndio wanufaika wa kubwa na mradi huo ni wao, pia TARURA iendelee kutoa huduma na maeneo mengine yenye uhitaji hasa kipindi cha masika barabara ziweze kupitika wakati wote.