Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Morogoro

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya OR-TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu  Mhandisi. Rogatus Mativila ameitaka Wakala ya barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) mkoa wa Morogoro kuongeza umakini kwa wakandarasi waotekeleza miradi ya Ujenzi wa barabara na madaraja ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa ubora na viwango vinavyotakiwa.

Mhandisi Mativila ameyasema hayo leo wakati wa Ziara yake ya kikazi ya kukagua miundombinu ya barabara na madaraja zilizoathiriwa na mvua Wilaya ya Morogoro.

Amesema kwamba miundombinu hiyo ikikamilika kwa ubora kutasaidia kuimarisha uchumi kwa wananchi wa maeneo husika.

“Maono ya Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wanachi wa vijijini wanaondokana na changamoto ya Barabara hasa katika kipindi cha mvua”.

“Mhe. Rais anatoa Fedha nyingi za Ujenzi wa Barabara na madaraja ili miundombinu hii iweze kuwa imara sasa inapotokea wakandarasi wanafanya chini ya kiwango haipendezi, sasa niwaombe TARURA muongeze umakini katika kulisimamia hili”.Aliongeza

Aidha, Mhandisi Mativila alionesha furaha yake kwa kuona Ujenzi wa Barabara ya Tegetero mpaka Lubwe yenye kilometa 1.0 inayojengwa kwa kiwango cha zege na kusema imetendewa haki.

Kwa upande wake Meneja wa Wilaya ya Morogoro Mhandisi Enock Waitara amesema mradi wa Ujenzi wa barabara ya Tegetero mpaka Lubwe itaghatimu kiasi cha shilingi milioni 577 hadi kukamilika kwake na itasaidia kuimarisha uchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

Please follow and like us:
Pin Share