Video Queen maarufu nchini Tanzania, Agness Gerald maarufu kama Masogange amefariki dunia jioni ya leo Aprili 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, jijini Dar es salaam.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na ndugu wa karibu na marehemu, Dick Sound ambaye amesema mwili wa marehemu unasafirishwa jioni hii kwenda kuhifadhiwa mochwari- Muhimbili.

Wiki tatu zilizopita marehemu alishindwa kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi iliyokuwa ikimkabili kwa kulazwa hospitalini, hii ni kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu wiki iliyopita.

Mastaa mbalimbali wa muziki na waigizaji wa filamu wametoa pole kufuatia taarifa hizo za mshtuko za kifo hicho, na Bongo5 inatoa pole kwa familia yake katika kipindi hiki kigumu.