Na Magrethy Katengu,JamhuriMedia
Dar es Salaam

Tanzania Miongoni mwa Nchi kinara kwa uzalishaji Madini ya Kinywe(Graphite) Afrika inashika nafasi ya 3 ambapo huzalisha kwa asilimia 0.64 kwa mahitaji yote Duniani nafasi ya pili ikifutiwa na Msumbiji 10% huku nafasi ya kwanza ni Madagaska ambao huzalisha 13% .

Akizungumza leo Novemba 20, 2024 Jijini Dar es salaa Waziri wa Madini Anthony Mavunde
wakati wa uzinduzi kitabu cha madini ya viwandani ktoleo la pili kilichoandaliwa na taasisi ya utafiti ya Madini( Jiologia GST) kilichoelezea maeneo yanapopatikana hayo madini matumizi yake pia taarifa za kitafiti kwa miaradi ambayo imeshaanza kuzalisha na hatua za uendelezaji baadhi ya maeneo.

Tanzania ina aina mbalimbali za madini ya viwandani ambapo kwa mujibu wa toleo jipya la pili la kitabu cha madini viwandani kilichoandikwa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kimeonesha aina 43 za madini viwandani ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda na ufungamanishaji wa sekta za kiuchumi nchini.

Waziri Mavunde amefafanua kuwa, kitabu cha madini ya viwandani kinaonesha aina za madini 43 yakiwemo madini ya Kinywe,Jasi, Chokaa, Lithium, Helium, Manganese, shaba, chuma, ulanga na mchanga mzito wa baharini pamoja na madini mkakati.

Waziri Mavunde akifafanua Madini ya Kinyw e amesema madini hayo yamekuwa na uhitaji mkubwa Duniani husaidia kutengeneza betri za magari ya Umeme na mahitaji yake kwa mwaka ni takribani ni tani Milioni sita na laki tano lakini huzalishwa Tani Milioni 1.2 kwa mwaka huku Nchi ya China ndiye Mzalishaji mkubwa kwa asilimia 64% Duniani.

“Tanzania tunayo Miradi zaidi ya saba ya Madini Kinywe ambayo haijaanza iko katika hatua ya mwisho na ikianza itaitoa katika nafasi ya chini na kusogea hadi nafasi ya juu” amesema Waziri

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa GST , Dkt. Mussa Budeba amewakaribisha wadau wa Sekta ya Madini kutumia taarifa inazochapisha ili kupata uhakika wa taarifa kuhusu mahali halisi madini yanapopatikana nchini kupitia kitabu hiko kilichozinduliwa kimeainisha aina 43 ya na mahali yanapopatikana.

Hata hivyo Dkt Budeba amesema huo ni muendelezo wa kuisaidia Serikali na wanapofanya tafiti zao wanaziandika katika mfumo wa taarifa ili kusaidia pia na wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi wanaokuja kuwekeza.

Dkt.Budeba ameongeza kwa toleo hilola kitabu cha madini viwandani, GST ina ramani na machapisho mbalimbali yanayoelezea upatikanaji wa madini kupitia utafiti wa jiolojia, jiofiziki na jiokemia.

Kwa mujibu wa utafiti, Tanzania ina aina mbalimbali za madini ambayo kwa mfumo wa makundi yakiwemo , madini ya viwandani , madini ya vito, madini ya metali, madini mkakati , madini adimu (REE), na madini ya nishati.

Aidha GST ilianzishwa rasmi mwaka 1925 na Ukoloni wa Mwingireza wakati huo ikiitwa British Oversee Management Authority yaani (BOMA).