Tanzania imetajwa kuwa nchi ya Tano Kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa selimundu (Sickle Cell) Duniani ambapo Kwa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Cha Sayansi na Tiba Shirikishi (MUHAS) katika mikoa mitano ambapo zaidi ya wagonjwa 70000 wanapatiwa huduma katika vituo vya Afya.
Akizungumza wakati wa zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kusaidia matibabu ya kubadilisha damu kwa wagonjwa wa Sikoseli lililoandaliwa na ubalozi wa Ufaransa na (MUHAS) msimamizi wa mradi wa Sikoseli na Mhadhiri wa chuo cha MUHAS Profesa Emmanuel Balandya amesema wamefanya tathmini kwa miaka 20 tangu programu za Sikoseli zianzishwe nchini.
Amesema mahitaji ya damu ni makubwa kulingana na tatizo lilivyo nchini hivyo wanahitajika wachangiaji wengi nchi nzima ili kuhakikisha wanaweza kuwasaidia wagonjwa wengi zàidi.
“Katika mikoa minne Kuna wagonjwa 7000 tumejitahidi kukutana nchi nane ili kujadiliana kwa pamoja jinsi ya kutatua tatizo la Sikoseli pamoja na kufanya tafiti za vinasaba” amesema.
Kwa upande wake Dk Elisha Osati Mwenyekiti Mwenza wa mtandao wa magonjwa ya Sikoseli nchini (TSDA) amesema asilimia 1.2 ya watanzania wanavinasaba vya ugonjwa huo ambapo watoto 11000 kila mwaka wanazaliwa wakiwa tayari na ugonjwa.
Amesema hali hiyo ndio. Imepelekea ongezeko kubwa la wagonjwa na kuifanya nchi kuwa nafasi ya nne Afrika kuwa na wagonjwa wengi lakini ya Tano Duniani.