Na Shamimu Nyaki – WUSM
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa, Aprili 24, mwaka huu, Wizara kwa kushirikiana na Bodi ya Filamu inatarajia kusaini makubaliano Maalum (MoU) na Wataalam kutoka Korea Kusini kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa uanzishwaji wa Shule ya Filamu hapa nchini.
Chana amesema hayo Mlimani City Dar es Salaam wakati akizindua Filamu ya The Green Tanzanite ambapo ameipongeza Kampuni ya Dar Squard chini ya uongozi wa Salman Bhamra kwa kufanikisha uandaaji wa filamu hiyo ambayo inatarajiwa kutazamwa ndani na nje ya Tanzania.
“Katika kipindi cha cha Uongozi wangu nitahakikisha Filamu za Tanzania zinapata nafasi katika mashirika ya ndege pamoja na kuingia makubaliano na Waandaji wa Filamu wa Kimataifa” amesema.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya kutengeza filamu bora ambazo zitaleta ushindani soko la ndani na nje.
Huku Muandaaji wa Filamu hiyo Bhamra akieleza kuwa Kampuni yake itaendelea kutumia vijana wa kitanzania katika kutengeneza filamu kutakwenda Netflix tunatengeneza local content kwa ajili ya Watanzania
Filamu hiyo imekua ya kwanza kutoka Afrika Mashariki kuoneshwa kwenye kumbi za Sinema katika Jamhuri ya Czech.