Tanzania inatarajia kuungana na nchi zingine duniani kwenye kuadhimisha siku ya Malaria Duniani ambayo ufanyika April 25 kila mwaka.
Maadhimisho hayo ya kitaifa yatafanyika wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma huku Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii akitarajiwa kuzindua ripoti ya hali ya Malaria nchini.
Akiongea jijini Dar es Salaam leo, Waziri Nyoni ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi kutoka VectorWorks alisema kutakuwa na shamra shamra mbali mbali kuanzia tarehe 22 April kabla ya kufikia kilele cha maadhimisho hayo.
VectorWorks ni mradi wa miaka mitano wa kupamba na malaria hapa nchini umefadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani – USAID kupitia Mfuko wa Raisi wa Marekani wa kudhibiti malaria na kuratibiwa na John Hopkins Center for Communications.
‘Sisi kazi yetu ni kuhakikisha hali ya ugonjwa wa malaria inapungua. Kwa sababu hiyo, tumekuwa na zoezi endelevu la kugawa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa kila kaya hapa nchini. Vile vile, tunatumia vituo vya afya kuwafikia walengwa wakuu ambao ni akinamama waoenda kliniki na watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja, alisema Nyoni.
Akina mama wanaonza kliniki ni lazima wapatiwe chandarua chenye dawa ya muda mrefu bure. Hii njia bora ya kujikinga na mbu waenezao malaria. Vile vile tunafanya kazi kwa kushirikiani na Serikali kupitia Wizara ya Afya kitengo cha kupamba na Malaria nchini ambao wamekuwa wakipuliza dawa yenye viatilifu kwenye maeneo yenye masalia ya mbu. Tumepiga hatua kubwa kupunguza malaria hapa Tanzania kwa hivyo natoa wito wangu kwa kila Mtanzania kuhakikisha analala kwenye chandarua kwenye dawa ya muda mrefu, aliongeza Nyoni.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni mimi natokomeza malaria, wewe je?