Mpaka wa Tunduma unaounganisha mataifa ya Tanzama na Zambia ndio wenye pilikapilika nyingi kati ya mipaka yotenchini.

 Hii inatokana na ukweli kuwa mpaka huu ndio unaopitisha asilimia kubwa yaa shehena inayoshushwa katika Bandari ya Dar es Salaam kwenda mataita ya kusini mwa Afrika, hasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)Kuna biashara kubwa inafanyika hapa Tunduma ikiwaingizia kipato maelfu ya Watanzania, hivyo kuchangia katika uchumi wa taifa,” anasema ofisa mmoja wa Uhamiaji mpakani Tunduma.

 Barabara inayochagiza uchumi wa lunduma na wa taifa zima ni ile inayotahamika kama TanZam (Tanzania Zambia Highway) inayotoka Dar es Salaam kupitia Morogoro, lringa, Mbeya hadi Songwe.

“Ni þarabara inayohudumiwa na TANROADS (Wakala wa Barabara nchini). Pamoja na matengenezo, pia TANROADS inadhibiti ubora wake kwa kusimamia mizani,” anasema Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Songwe, Suleiman Bishanga.

 Kipande cha barabara hii kipo mkoani Songwe na kwa maana hiyo kinaangukia kwenye usimamizi wa Bishanga huku pia mizani ya mwisho kabla ya kuvuka mpaka wa Tunduma ikiwa eneo la Mpemba ndani ya mkoa huu.

 Mizani za barabarani ndizo mlinzi’ muhimu wa barabara na mbali ya kupima uzito wa shehena Zinazopita, pia hutoa takwimu sahihi Zinazowezesha kutathmini mwenendo

 wa uchumi wa taifa na kiasi cha shehena kinachosafirishwa na kulipiwa ushuru kila siku.

“Changamoto zinazotokea hapa Tunduma sisi (TANROADS) huwa tunaitwa na kushirıkishwa kutafuta suluhu.” Mara zote suluhu imepatikana na tunazidi kuboresha miundombinu kuhakikisha kuwa Watanzania wananufaika na biashara inayofanyika hapa, anasema Kaimu Meneja Bishanga.

 Hata hivyo, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kwamba tatizo la mpaka huu kwa upande wa Tanzania linachagizwa na uduni wa miundombinu upande wa Zambia. Mmoja wa madereva wa magari makubwa aliyezungumza na gazeti hili, Maneno Magasha, anasema barabara za Zambia ni finyu na chakavu

 “Ni kama hawa jamaa (Zambia) hawapendi namna tunavyonufaika na mpaka huu ndiyo maana hawaonyeshi dalili ya kuboresha mundombinu upande Wao, anasema Magasha.

 Anasema wakati malori ya mafuta yakipita haraka mpakani, yale yenye makontena huchukua muda mrefu ande wa Zambia katokana nakutokuwapo kwa zana bora na za kisasa.

JAMHURI linafahamu kwambakati ya asilimia 90 hadi 95 ya shehena inayopita Tunduma huelekea DRC hivyo kutounufaisha moja kwa moja uchumi wa Zambia, huku pia sehemu kubwa ya malori yanayobeba shehena hiyo yakimilikiwa na wafanyabiashara wa Tanzania.

“Nadhani ni vemą wakubwa wakazungumza na wenzao wa Zambia ili kama hawawezi kuboresha walau barabara na maegesho kwa upande wao, kazi hiyo ifanywe na Tanzania, kwa kuwa ni sisi ndio tunanufaika zaidi,” anasema.

 Profesa Mbarawa azungumza Akizungumzia msongamano wa malori uliopo Tunduma na hatua zinazochukuliwa, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa anasema ni suala la muda tu.

 “Tayari W1zara imetangaza ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Igawa -Songwe Tunduma yenye urefu wa kilomita 218 kwa kutumia mfumo wa EPC+F (Engineering, Procurement, Construction and Financing)Tunaanmini ujenzi wa barabra hi utakapokamilika, utapunguza au hata kuondoa kabisa msongamano huo,” anasema Profesa Mbarawa.

 Profesa Mbarawa anakiri kufahamu uduni wa miundombinu ya upande wa Zambia, lakini anasisitiza kuwa badala ya kusaidia au kufanya ujenZi upande wa huko, ni vema kuimarisha kwanza barabara za upande wa Tanzania.

 “Ninaamini wakiona sisi tumejenga 4-lanes na wao wataanza hapo kwa 2-lanes’ Wamejitokeza makandarası wanane wanaoonyesha nia ya kuanza kujenga barabara hii,” anasema.

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Waziri Kindamba, wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara mkoani Songwe mbele ya Profesa Mbarawa aliwahi kushauri serikali ianzie Tunduma kutekeleza ujenzi wa barabara ya njia nne kuja lgawa badala ya kuanzia Igawa kwenda Tunduma.

 Kwa upande mwingine, Profesa Mbarawa anasema amezungumza na waziri mwenye dhamana kwa upande wa Zambia ili kuona namna ya kutatua tatizo la kifaa cha kukagua mizigo ‘scanner ambapo kwa upande wa Zambia wanayo moja tu, hali inayosababisha magari kusongamana kwa wingi yakIsubiri kukaguliwa.

 Naibu Waziri apigilia msumari Akizungumza na jarida linalomilikiwa

 na TANROADS kuhusu namna serikali livyojizatiti kuimarisha miundombinu Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na maeneo mengıne nchini, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, MhandisI Godfrey Kasekenya, anasema makandarasi wapo kazini na utekelezaji unaendelea vema.

 “Kwa hiyo ni muhimu kwa mameneja wa TANROADS mikoa yote kuweka kipaumbele katika kutengeneza maeneo korofi (ya barabara na madaraja) yaweze kupitika mwaka mzima na kuchangia uchumi wa taifa.

 “Hii ni kwa sababu barabara ni kichocheo cha kukua kwa sekta nyingine na ndiyo maana serikali itahakikisha inajenga na kukarabati maeneo yote “korofi’ ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji,” Miongoni mwa maeneo ya namna hiy0 ambayo yameshughulikiwa vema na TANROADS Mkoa wa Songwe ni miradi iliyopo ndani ya Wilaya mpya ya Songwe. Mmoja kati ya miradi mikubwá ni daraja la kisasa linalounganisha vijiji vya Galula na Mheza kwenye Mto Songwe, vijiji maarufu kwa kilimo cha mpunga, maharage na alizeti.

 Kwa sasa wananchi wanatumia daraja la muda wakisubiri kukamilika kwa ujenzi wa daraja litakalogharimu Sh bilioni 2 Desemba mwaka huu.

 Kazi nyingine iliyofanywa na TANROADS Songwe inayostahili kupigiwa mfano ni ujenzi wa tuta lenye urefu wa kilometa tano katika Mbuga ya Tulila kuzuia mafuriko yaliyosababıshwa na kubomoka kwa kingo za Mto Zira mwaka 2019. Adha hi lisababisha madhara makubwa kwa wakazi wa vijiji vya Kanga na Mbala baada ya kukatika kwa mawasiliano ya barabara.

 “Huwezi kuamini. Hapa tulikuwa tukivuka kwa mitumbwi, tena kwa nauli kubwa hata kuliko ile ya kwenda Mbeya mjini,” anasema Shida Mwamanda, mkazi wa Kanga na kuongeza kuwa, kwa upande mwingıne, wakazi wa Mkwajuni, makao makuu ya Wlaya ya Songwe, walikwenda Mbeya mjini kwa kutumia barabara ya Chunya yenye mzunguko mrefu.

 Shida anasema mafuriko hayo yalimtia hasara kubwa yeye binafsi kwani alipoteza shamba la mahindi lenye ukubwa wa ekari nne. “Mazao yetu yalisombwa na mafuriko na kujikuta ghafla tukiishi maisha magumu,” anasema Shida.

 Nauli ya kuvuka kipande hicho kwa mtumbwi ambao S1 salama ilikuwa Sh 7,000 kwa mtu mzima na Sh 2,000 kwa watoto. Mara moja TANROADS ikaingilia kati na kuinua tuta la barabara eneo la mbuga kwa kumwaga kifusi, kisha kujenga makaravati saba kuruhusu maj kupita kwa urahisi bila kuathiri barabara.

 Nyanda za Juu kufunguka zaidi Kwa mujibu wa jarida la TANROADS, Naibu Waziri Kasekenya  

anasema serikali itajenga Barabara va Iringa hadi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye urefu wa kilomita l04) kwa kiwango cha lami kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia (WB).

UjenzI wa barabara hiyo utaimarisha na kukuza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania. “Ujenzi utakapokamilika, utawarahisishia watalii kufika hifadhini,” anasema Kasekenya.

 Hifadhi nyingine iliyopo Nyanda za Juu Kusini inayotarajiwa kuunganishwa kwa barabara ya kisasa ni Kitulo iliyopo Makete, mkoani Njombe, itakayounganishwa na Mkoa wa Mbeya.

 Kwa upande mwingine, Naibu Waziri huyo anasema kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inaendelea ikiwa ni hatua za maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Ruanda-Ilyula – Nyimbili (km 21) na Katumbasongwe – Kasumulu – Ngana Ileje (km 90.1) kwa kiwango cha lami.

 “Mipango ya aina hii itaendelea katika maeneo mengine ya Nyanda za Juu Kusini na Tanzania nzima, kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuifungua nchi kupitia ujenzi wa miundombinu ya barabara za kisasa,” anasema. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini pia itaunganishwa kwa lami na mikoa ya katikati ya nchi kuelekea magharibi; yaani Singida na Tabora, hivyo, mbali na utalii wa ndani kukuza pia shughuli za kiuchumi kama Kilimo na uchimbaji madini.

 Kasekenya anasema ukubwa wa gharama zinazotumika kujenga miundombinu hii kunawafanya wananchi Kuwa na jukumu la kuilinda idumu kwa muda mrefu.

Mativila amshukuru Rais Samia

Kwa upande mwingine, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila, amenukuliwa akisemna mafanikio yanayopatikana yanatokana na utendaji bora wa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Anasema Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kutoa fedha za makandarasi kwa wakati maeneo mbalimbali ya nchi, ndiyo maana miradi mingi inatekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.

 “Utendaji wetu unakwenda vizuri kwa kuwa tunapata ushirikiano mkubwa kutoka serikalini kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuleta mabadiliko sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara.Mativila anakiri kushuhudia mabadiliko makubwa tangu Rais Samnia alipomteua kushika nafasi hiyo Julai 28, mwaka jana.

“Nilipoteuliwa na kuingia ofisini nilichukua vitu vitatu na kuvipa msukumo wa kuvisimamia katika utekelezaji. Kwanza, Bajeti ya Serikali; lani ya Uchaguzi (ya CCM) na Dira ya Maendeleo ya Taifa,” anasema.

 Songwe, mkoa wa kimkakati

Songwe ni miongoni mwa mikoa inayozalisha chakula kwa wingi nchini,ukitajwa kuwa lango la uchumi wa nchi ambapo asimilia 72 ya mizigo Inayosafirishwa kwenda mataifa ya Zambia, DRC na Malawi hupita katika mipaka iliyopo mkoani humo, ule wa Tunduma wilayani Momba na wa Isongole uliopo lleje

 Kwa mantiki hiyo, barabara za Songwe Zinapaswa kuwa imara na zinazopitika

kwa mwaka mzima ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla; kazi ambayo inasimamiwa na TANROADS Mkoa.

 “Madaraja na barabara hizi Zinaiunganisha Songwe na mataita ya Zambia na Malawi pamoja na mikoa ya Mbeya na Rukwa,” anasema Mhandisi wa TANROADS, Joseph Homvye.

 Uimara wa barabara hizo na uwezekano wa kupitika kwa mwaka mzima kunawapa fursa wakulima wa Songwe kusafirisha mazao yao na kuyapeleka kwenye masoko.

 Takwimu zinaonyesha kuwa Songwe, mkoa wenye wilaya nne; Mbozi, lleje, Songwe na Momba, huzalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara, ukiwa ndani ya ‘tatu bora’ sambamba na mikoa ya Ruvuma na Rukwa. Mazao haya, pembejeo na rasilimali watu hufika kila Zinakotakikana kutokana na ubora wa mtandao wa barabara zinazosimamiwa na serikali, zikiwamo zile zlizo chini ya TANROADS.

unaotenganisha nchi za Tanzania na Malawi. Wakazi wa Isongole na Ileje kwa ujumla wameupokea mradi huu kwa mikono miwili, wakikumbuka adha waliyokuwa wakikutana nayo awali hasa nyakati za mvua. Mkoa wa Songwe wenye mlima mirefu upande mmoja, hupata mvua nyingi za masika, hivyo maji yanayotiririka kutoka milimani kujaza mito na vijito na kufanya ujenzi wa madaraja na barabara kufanywa kwa ustadi mkubwa.

 “Haikuwa rahisi kusafirisha mizigo mikubwa au kwa wingi. Barabara ilikuwa mbaya sana,” anasema Viçtor Nyondo, dereva wa bodabda raia wa Malawi mkazi wa Chitipa, Malawi.

 Kazi yakeni kuvusha abiria kutoka Chitipa kwenda katika Soko la Isongole kufanya biashara.

 Anasema tangu kumalizika kwa barabara, idadi ya wateja wake imeongezeka.

 “Kwetu (Malawi) tunalima sana alizeti na soya. Zamani soko lilikuwa dogo, lakini sasa tumepata soko la uhakika Isongole ambapo wafanyabiashara wakubwa hufika,” anasema Nyondo.

 Barabara ya Mpemba hadi Isongole haikuwa ikipitika kwa urahisi nyakati za masika kutokana na mito kujaa.

 Lakini sasa hata magari madogo aina ya Pro- Box yameongezeka yakisafirisha mizigo kutoka Tunduma kupeleka Malawi kupitia mpaka wa llomba.

 Mhandisi Homvye anasema ujenzi wa barabara ya Mpemba hadi Isongole

umehusisha ujenzi wa daraja la watu na magari katika Mto Songwe kuelekea mpaka wa lomba.

 “Mpaka wa llomba si maarufu sana kama ule wa Kasumulu uliopo Kyela- mkoani Mbeya ambao kuna mpango wa kuuunganisha na Songwe. Kwa sasa serikali imo katika hatua za upembuzi yakinifu kuiunganisha Barabara ya Isongole I na vijji vya lleje hadi Kasumulu,” anasema Mhandisi Homvye.

 Ujenzi wa madaraja na makaravati

 Mkoa wa Songwe una mito mingi mikubwa na midogo, ikiwamo miwili inayobeba jina moja “Songwe’, mmoja

 ukianzia katika milima ya Loleza, Mbeya na kumwaga maji Ziwa Rukwa, na mwingine ukianzia milima ya Tunduma na kwenda kumwaga maji Ziwa Nyasa.

 Uwepo wa mito na vijito hivi kunawapa TANROADS kazi kubwa ya kujenga madaraja na makalavati ili kuhakikisha shughuli za Watanzania Zinaendelea bila kikomo.

 Katika Wilaya ya Ileje, TANRAOADS Mkoa wamejenga makaravati kuziunganisha barabara zote ziweze kupitika kwa muda wote.

 Ujenzi wa Daraja la Nakambekeswa linalounganisha miji ya Itumba na Isongole, umekamili na sasa linapitika bila shaka kwa mwaka mzıma, likiondoa adha waliyokuwa wakikumbana nayo wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ileje nyakati za mvua. Mradi mwingine ni

ujenzi wa karavati la milango miwili katika barabara ya Kasumulu kupitia Kijji cha Ndembo, ikitajwa kurahisisha usafiri na usafirIshaji kwenda Kasumulu kutoka Mpemba, Songwe.

 Mkazi wa Ndembo, Odian Mbalwa, anasema upanuzi wa daraja hilo umeongeza idadi ya watumiaji wa Barabara ya Kasumulu.

 Anavitaja vijiji vya Ndembo, Kafwafwa na Isoko kuwa miongoni mwa vijiji vitakavyonufaika zaidi.

 “Hata Soko la Ndembo nalo litapata bidhaa nyingi kutoka Malawi. Awali wafanyabiashara wengi walikuwa wakishindwa kuleta mizigo kwa sababu ya ufinyu wa daraja.

 “Mwanzoni lilikuwapo daraja la jeshi (madaraja ya chuma). Lilikuwa finyu sana hata pikipiki zisingeweza kupishana. Lakini sasa magari yanapishana. Hata wafanyabiashara kutoka Kasumulu na Kyela waliokuwa wakilazimika kupita Tukuyu hadi Mbeya kwenda Songwe au Tunduma, sasa watapita hapa,” anasema Mbalwa.

 Juma Minja, mkazi mwingine wa Ndembo, anasema kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili kutamaliza tatizo la maji ya kijito jirani kusambaa na kuingia kwenye makazi ya watu.

 “Ukikatazama hapa huwezi kufahamu, lakini mvua ikinyesha ilikuwa ni shida kubwa, hakuna kupita,” anasemna Minja, akiwapongeza TANROADS Mkoa wa Songwe kwa kuimarisha miundombinu mbalimbali.