Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Pwani

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani, kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2024 imefanikiwa kuzuia mfumo wa ukusanyaji wa michango ya waajiri ambao wamekuwa hawapeleki michango ya waajiriwa wao katika mifuko ya Hifadhi ya Jamii ikiwemo NSSF ikiwa ni takwa la kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 13, 2024, Naibu Mkuu TAKUKURU, Mkoa wa Pwani Ally Sadick, amesema uzuiaji huu ulifanyika Baada ya kuwatafuta waajiri Sabini na Saba (77) ambao walikuwa na jumla ya deni la Michango ya sh. 7, 505,723,317.10, Baada ya Taasisi hiyo kuingilia kati kuhusu ukusanyaji wa Michango ndipo wadaiwa na NSSF wakakubaliana kuwa ifikapo Julai 2024 wafikie 20% ya deni lote.

Aidha TAKUKURU ilifuatilia kwa kusimamia Sheria za mifuko ya hifadhi pamoja na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 , ambapo makusanyo yalifikia sh. 1, 543,125,427,00/= tarehe 17, Julai 2024 na kuwa na makubaliano yalifikiwa Kwa 103%.

Hata hivyo, Waajiri hao 77 wamesema wapo tayari Kwa kushirikiana na TAKUKURU Katika kuendeleza Mapambano dhidi ya Rushwa Kwa kuwa hawakuwa na Elimu ya makosa ya Rushwa Kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini na Makosa ya hifadhi ya Jamii.

Pia, Katika ufuatiliaji huo TAKUKURU ilibaini baadhi ya waajiri hao hawakuwa wanajua kuwa kutokupeleka Michango kwa wakati NSSF ni kosa kisheria, Baadhi ya Waajiri walikuwa hawapeleki Michango Kwa makusudi hivyo kusababisha kuvunja Sheria , Kwani mara TAKUKURU kuwapa Maelekezo walichanga bila shida.

Ameendelea kwa kusema, Nia ovu ya baadhi ya waajiri Ili kupoteza Fedha za watumishi wao na kujinufaisha kwa kutowalipa Michango NSSF na baadae kutopata mafao kama stahili ya watumishi.

Kwa upande wa Taasisi hiyo Kwa kipindi hiki wamefanya Semina 53, Mikutano ya hadhara 39, vipindi vya Redio 3, Kuimarisha klabu za wapinga rushwa 53, Uandishi wa Makala 8 na TAKUKURU rafiki 3.

Ameongeza kuwa Katika kipindi Tajwa TAKUKURU Mkoa wa Pwani imeendelea na Utekelezaji wa Program ya TAKUKURU Rafiki na kuzifikia jumla ya Kata Sita (6). Kero zilizoibuliwa na kupatiwa ufumbuzi zilizotoka idara ya Ruwasa, Halmashauri, Afya, TFS, Elimu na TANROADS.