Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia
Dar es Salaam
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kinondoni imesema katika kipindi cha mwezi Okoba hadi Desemba 2024 wamefanya uchambuzi wa mifumo na wamebaini mianya ya rushwa katika maeneo ya ofisi, taasisi, na idara na ambapo kuna upotevu fedha na ufujaji fedha na baadhi ya wananchi kuonewa kutokana na elimu juu ya mifumo iliyopo
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 6 ,2024 Dar es Salaam Mkuu wa TAKUKURU1 Kinondoni Christian Nyakizee amebainisha kuwa wamefanya uchambuzi mifumo wa usimamizi na ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki ( POS) katika Manispaa na kubaini baadhi ya watumishi kutowasilisha fedha za makusanyo katika akaunti ya Serikali.
Pia wahasibu wa Halmashauri kutofanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa wakusanyaji ushauru na wakati mwingine ukaguzi kufanyika baada ya muda mrefu hivyo kusababisha mapato kupotea na fedha kufujwa.
” Tulibaini qatumishi kutowasilisha fedha za makusanyo hawachukuliwi hatua stahiki pale wanapobainika na wasio waaminifu ambao tulibaini wanagushi stakabadhi kwa kuandika kiasi kidogo kuliko kiasi halisi walichopokea kutoka kwa wateja” amesema Nyakizee.
Sanjari na hayo Takukuru waliendelea na Uchambuzi wa mifumo na usomaji wa Mita za Ankara za maji Dawasa Wilaya ya Ubungo na walibaini taarifa za malalamiko kutoka kwa wateja na zinapopokelewa zinachukua muda mrefu kushughulikiwa na baadhi ya Mita ni chakavu hutoa taarifa zisizo sahihi nyingine zimesimama hazisomi huku nyingine zikiwa na ukungua hivyo haziomeka vizuri na kupelekea msoma Mita kusoma pasipokuwa na uhakika .
Hata hivyo Nyakizee amebainisha kuwa walifanya Uchambuzi wa mfumo wa uondoshaji taka ngumu ngazi ya Kaya maeneo ya biashara katika Manispaa ya Kinondoni na walibaini Vyombo vya kukusanyia taka maeneo mengi ya Halmashauri hiyo havitoshelezi na idadi kubwa ya Kaya hawahifadhi taka kwenye makasha wanahifadhi kwenye viroba na hawana elimu kabisa ya utenganishaji wa taka laini na taka ngumu
Katika hatua nyingine Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Kinondoni katika kipindi hiko wamefanikiwa kufuatilia miradi yenye thamani ya Tsh bilioni mbili iliyohusu sekta ya elimu na kukuta mapungufu ikiwemo kubadilishwa kibali cha awali.
Christian Nyakizee amesema walifuatilia miradi mitano yenye thamani ya zaidi ya bilioni mbili katika ya miradi hiyo miwili ni yenye thamani ya Tsh 144,8000,000 imekutwa na mapungufu madogo madogo na wahusika walishauriwa kurekebisha mapungufu hayo.
“Katika mradi mmoja wa ujenzi wenye thamani ya Tsh 90,000,000 ulibainika kubadilishwa kibali ikwani kibali cha awal kilichotolewa kilikuwa ni cha kufanya ukarabati wa majengo madarasa badala yake wakaanzisha Ujenzi upya ambapo kufanya hivyo ni kosa kisheria kubadili matumizi ya fedha bila kibali kutoka sehemu husika hivyo ofisi inaendelea na ufutiliaji wa kina wa suala hili ” amesema Nyakizee
Hata hivyo walipokea malalamiko 85 na kati ya hayo malalamiko 46 yalihusu rushwa na 39 hayakuhusu rushwa na walalamikaji wengine wamewashauri wakafungue majalada na wengine wapeleke malalamiko Yao sehemu sahihi yakashughulikiwe katika hatua mbalimbali
Pia katika kipindi husika Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru Kinondoni wamefungua mashauri 6 Mahakama ya Halmashauri ya Kinondoni na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo na Jamuhuri imeshinda mashauri mawili