Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi imebaini kuwepo kwenye miradi iliyotekelezwa katika Halmashauri mbalimbali za mkoa huu ikiwa na upungufu wa zaidi ya Shilingi Bilioni 2.1 na wameweza kuchukua hatua mbambali kwenye miradi hiyo.
Hato yamesemwa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Katavi Stuart Kiondo wakati alipokuwa akitowa taarifa kwa wandishi wa Habari ya utekelezaji wa kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu yakuanzia Oktoba hadi Desemba 2022.
Amebainisha kuwa TAKUKURU Mkoa wa Katavi katika kipindi hicho cha miezi mitatu ya Oktoba na Desemba mwaka 2022 wameweza kufatilia miradi yenye thamani ya shilingi Bilioni 5 katika sekta za ujenzi,elimuna afya .
Katika ufatiliaji huu wa miradi kwenye Mkoa huu wameweza kubaini miradi yenye thamani sh.2,170,000,000 ikiwa na mapungufu kwenye miradi iliyotekelezwa katika Halmashauri mbambali za Mkoa huu.
Kiondo amesema kati ya shilingi Bilioni 5 zilizotolewa kati hiyo shilingi Bilioni 1. 12 zilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan zijulikanazo Pochi la Mama .
Fedha hizo ambazo zilitumika kujengea jumla ya madarasa 55 katika shule 25 madarasa ambayo yamekamilika na yameanza kutumika .
Naibu Mkuu huyo wa TAKUKURU ameitaja baadhi ya miradi hiyo ni miradi yenye upungufu ni mradi wa ujenzi wa jengo la ICU na nyumba za watumishi, Hospitali ya Wilaya ya Tanganyika yenye thamani ya s.,340,000,000 miradi hiyo ilikutwa na mapungufu ya matofali yasiyo na kiwango na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi na tayari uchunguzi umeanza .
Ujenzi wa kituo cha Afya Itenka Halmashauri ya Nsimbo wenye thamani ya wenye thamani ya sh.530,000.000,ujenzi wa jengo la dharura Hospitali ya Halmashauri ya Nsimbo sh.300,000,000 na ujenzi wa majengo matano Bohari,mionzi jingo la utawala, jengo la mama na mtoto na jingo la kufulia nguo yenye thamani ya sh.1,000,000,000 Hospitali ya Nsimbo .
Amesema kasoro walizozibaini ni ukiukwaji wa taratibu za manunuzi na ucheleweshaji ambapo uchunguzi wake tayari umeanza na waliweza kubaini matofali matofali yalitumika kwenye ujenzi hayakuwa na ubora baadhi ya kuthibishwa .
Na wataendelea kufatilia kwa karibu fedha zote zinazotolewa na Serikali ili kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa na upande wa miradi kuwa bora na thamani ya fedha kuonekana .
Kiondo ameeleza kuwa katika kipindi cha robo ya kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu wanataraji kuongeza juhudi za kuimarisha kuzuia rushwa kwa kufatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhamasisha kutoa elimu kwa wananchi ya ushiriki wa kupiga vita rushwa .
Kiondo amewataka wananchi wa Mkoa wa Katavi kutoa taarifa mara moja pindi ambapo wanapokuwa wanapigiwa simu na watu ambao ni matapeli wanao kuwa wamewapigia simu na kujifanya wao ni Maafisa wa TAKUKURU kwa lengo la kuwatishia na kutaka kujipatia pesa.