TAKRIBAN watu 29 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel katika eneo la kati na kaskazini mwa Ukanda wa Gaza Jumamosi na usiku kucha, Shirika la habari la Reuters linaripoti likiwanukuu madaktari.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilianza mashambulizi mengine huko Jabalia wiki moja iliyopita, likisema Hamas ilijaribu “kurejesha” miundombinu yake huko.

Takribani Wapalestina 150 wameuawa huko kwa muda wa wiki moja iliyopita, kulingana na maafisa wa afya huko Gaza.

Watu waliokimbia makazi yao katika eneo hilo wanasema wanajeshi wa Israel wamezingira Jabalia na kuwaamuru kuondoka.

Kusini mwa Lebanon, Hezbollah inasema “ilipambana” na wanajeshi wa Israel wakijaribu kuhamia kijiji cha Ramiya, mapema Jumapili.

Wizara ya Afya ya Lebanon inasema watu 15 waliuawa katika mashambulizi matatu ya Israel jana Deir Bella, Al Maaysra na Barja.

Nchini Israel, IDF inasema Hezbollah ilirusha takribanI makombora 320 kutoka Lebanon hadi Israel siku ya Jumamosi.

Please follow and like us:
Pin Share