Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amekutana na jopo la wataalamu kutoka Taasisi ya Saratani Uganda (Uganda Cancer Institute).

Kiongozi wa Jopo la wataalamu hao Bw. Godfrey Osinde amesema kuwa wamekuja Tanzania kujifunza utendaji kazi kitengo cha tiba ya Saratani, Tiba Radiolojia pamoja na vipimo vya mfumo wa chakula (Endoscopy) kwa kuwa wapo mbioni kuanzisha kituo cha umahili cha Matibabu ya Saratani nchini mwao.

“Tumechagua kuja kujifunza Tanzania hususani Muhimbili kwa kuwa tunafahamu kuwa ni nchi ambayo ipo mbele katika eneo la matibabu ya kibingwa, lakini pia ina ukaribu wa kindugu na nchi yetu” amesema Bw. Osinde

Kwa upande wake Prof. Janabi amewaahidi kuwapa ushirikiano ili kufikia malengo yao.

Please follow and like us:
Pin Share