Jeshi la Magereza limeeleza kuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ pamoja na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiliwa huru kwa msamaha wa Rais uliotolewa katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Afisa Habari wa Jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje ameeleza kuwa katika maadhimisho hayo, Rais alitoa msamaha kwa wafungwa ambapo baadhi walitoka siku hiyo hiyo na wengine walibaki kumalizia muda wao, kutokana na kupunguziwa adhabu.
Amesema kuwa jumla ya wafungwa 585 kati ya 3,319 waliopewa msamaha waliachiliwa Aprili 26, mwaka huu.
Wafungwa 2,734 wakiwemo ‘Sugu’ na Masonga walibakia gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya msamaha wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Wawili hao walikuwa katika Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi (5) baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha ya kumkash Rais Dkt Magufuli.
Hukumu hiyo ilitolewa Februari 26 mwaka huu na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite baada ya na ushahidi wa upande wa mashtaka.