Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steven Mengere amewashauri wanaharakati na wanasiasa kufanya siasa za hoja na sera na si kutumia lugha za matusi na udhalilishaji lakini pia kutumia mitandao kutangaza biashara na vivutio vya nchi.
Hayo ameyasema leo wakati wakati akizungumzia mikakati ya taasisi hiyo lakini pia miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake.
Stevene amewashauri wanasiasa na wanaharakati nchini kufanya harakati na siasa za hoja na sera pasipo kumdhalilisha mtu mwingine kwani wapo badhi yao hutumia mitandao ya kijamii kama Twiter, Facebook, Istagramu .
“Taasisi yetu imeshindwa kuvumilia vitendo hivyo hivyo ni vyema sana kwa wanaharakati au wanasiasa kufanya siasa za kiistarabu kwani inasaidia kudumisha amani na upendo katika taifa hili,” amesema.
Amesema wamekuwa kwa mwaka huu wa 2024 wamejipanga kushirikiana na watu wa makundi mbalimbali wakimemo walemavu ambao wamekuwa wakisapoti juhudi za Rais Dkt Samia.
Amesema katika kusheherekea miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt Samia wameandaa tamasha kubwa ambalo watashirikiana vijana wa bodaboda na watu wenye ulemavu pamoja na kutoa mahitaji mbalimbali kwa watu wenye uhitaji lakini pia kufanya dua ya pamoja kwa ajili ya kuwaombea viongozi waliotangulia mbele ya haki na wananchi kwa ujumla.
Sambamba na hayo Mengere ametoka rai kwa wanaharakati na wanasiasa kufanya siasa za hoja na sera na si kutumia lugha za matusi na udhalilishaji lakini pia kutumia mitandao kutangaza biashara na vivutio vya nchi.
“Sisi kama taasisi hatutavumilia matusi na kejeli kwa Rais wetu nitoe rai tutumie mitandao hii ya kijamii kutangaza biashara lakini pia vivutio vyetu lakini sio kutafuta kiki kwenye mitandao kwa kuonyesha maisha ambayo si yako”amesema.
Ameongeza kuwa katika sekta ya michezo hivi sasa Tanzania inafanya vizuri na kuacha kuwa mtazamaji au mshirikina kwa sasa imekuwa mshindani mkubwa na hata kushindwa kwenye majukwaa makubwa.
Naye ,mwenyekiti wa wenye ulemavu, Adora Michael, amesema ni vyema taasisi ya Ongea na Mwanao ikawasaidia wazazi wenye ulemavu kwa kupata mahitaji muhimu kama sare za shule na kuwalipia baadhi ya mahitaji shuleni.
Kwa upande wake Susan Lewis ‘Mama Natasha’ amesema kuwa Taasisi ya Ongea na Mwanao inajujuisha wasanii mbalimbali ambao wanalenga kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule.