Spika wa Bunge la Ukraine Ruslan Stefanchuk, amesema Waziri wa Mambo ya Nje Dmytro Kuleba amewasilisha barua yake ya kujiuzulu .

Ukraine imekumbwa na wimbi la kujiuzulu mawaziri katika serikali ya rais Volodymr Zelensky.

Mawaziri wengine ambao pia wamejiuzulu ni Waziri anayehusika na usimamizi wa utengenezaji silaha pamoja na mawaziri wa viwanda, mazingira, sheria na naibu waziri mkuu.

Uamuzi huu wa kujiuzulu mawaziri ahwa ni baada ya Rais Zelensky kutaka kufanya  mabadiliko makubwa ya serikali yake wakati nchi hiyo ikiwa katika kipindi kigumu cha vita na Urusi.

Stefanchuk amesema ombi la kujiuzulu Waziri wa Mambo ya Nje litajadiliwa na  wabunge baada ya Rais Zelensky kusema kwamba Serikali yake inatarajia kufanya mabadiliko ili kujiimarisha na kupata matokeo yanayohitajika.

Please follow and like us:
Pin Share