Pamoja na zoezi la Usajili linalohusisha ujazwaji wa fomu za maombi pamoja na kuchukuliwa alama za Kibaiologia pamoja na Picha, Mkoa wa Songwe umeanza zoezi msingi la Mapingamizi ambapo wananchi wanapata fursa ya kuhakiki taarifa zao pamoja na kuweka mapingamizi kwa mtu yoyote wanayehisi si raia au si Mkazi wa eneo husika na amefanya usajili wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa, ambapo Bi. Coletha amewasihi Wananchi wa katanganyifu kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.
Zoezi hili lililoanza sambamba na kuendelea kwa usajili kwa Kata ambazo hazijakamilisha linahusisha Kata za ichenjezya, vwawa na mlowo Wilayani Mbozi mkoani Songwe baada ya kukamilisha hatua ya awali ya usajili.
Kwa mujibu wa Afisa Usajili Wilaya ya Mbozi Bi. Coletha Peter amesema zoezi hilo litahusisha wananchi wote wa mkoa wa Songwe na kuwataka kujitokeza kwa wingi kwenye mbao za matangazo ambako picha zote za waombaji wa Vitambulisho vya Taifa zimebandikwa pamoja na majina yao.
Amesema kama Mamlaka wamejipanga kuhakikisha wanapokea mapingamizi ya watu wote watakao bainishwa kwa njia ya wazi na siri na kuhakikisha Mamlaka inayafanyia kazi majina hayo mapema sambamba na kuanza uchakataji wa taarifa za waombaji wote waliokamilisha taratibu za Usajili ili vitambulisho vianze kutolewa kwa wakati.
“ Tumepanga siku 7 za mapingamizi ambazo ni fursa pia kwa wananchi kurekebisha taarifa zao iwapo watabaini kuna mapungufu yoyote na baada ya hapo hatutatoa nafasi tena ya mtu kurekebisha taarifa. Mbali na kurekebisha taarifa tunawaomba wananchi kuweka mapingamizi kwa wale wote ambao watakuwa wamesajiliwa na hawana sifa za kupewa vitambulisho vya Raia ili tuwaengue mapema kwenye mfumo” alisisitiza
Mkoa wa Songwe ni miongoni mwa mikao 16 ya Tanzania Bara inayoendelea na zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa na kwa Wilaya ya Mbozi mbali na kuanza mapingamizi Kata za Isandula, Itumpi, Kilimampimbi, ipunga na kata ya Itaka ndiyo zinaendelea na zoezi la Usajili kwa sasa.
Amesema baada ya kukamilika Kata hizo awamu ijayo itahusisha Kata za Nambizo, Magamba, Nanyala na Ruanda na kuwasititiza Wananchi ambao hawajafikiwa na zoezi kuvuta subira na kuendeela kujiandaa kwa zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa Viambatanisho msingi vinavyotakiwa katika zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu.
Mikoa mingine inayoendelea na zoezi la Usajili ni Mara, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Njombe, Iringa na Mbeya.
SOURCE: MICHUZI MATUKIO BLOG