Wenyeji, Singida Big Stars wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa LITI mjini Singida.
Mabao ya Singida Big Stars yote yamefungwa na nyota wake wa Kibrazil, Biemes Camo dakika ya 30 na Bruno Gomes kwa penalti dakika ya 80, wakati la Geita Gold limefungwa na Haruna Shamte kwa penalti pia dakika ya 45 na ushei.
Kwa matokeo hayo, Singida Big Stars inafikisha pointi 37 katika mchezo wa 19, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC ambao pia wana mechi moja mkononi.
Kwa upande wao Geita Gold baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 24 za mechi 19 nafasi ya saba.