MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadid ya Morocco, Simon Msuva, amewasili leo asubuhi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam.
Akitokea Morocco kwa ajili ya mapumziko mafupi baada ya ligi nchini humo kusimama Msuva amesema kuwa kwa Soka la Morroco lina ushindani mkubwa lakini anajitahidi kupambana ili kufikia hatua ya kucheza kimataifa zaidi.
Hata hivyo Msuva amesema kuwa changamoto kubwa inayomkabili ni lugha ambapo huko wanazungumza lugha ya kiarabu na kifaransa lakini kwa upande wake ana mwalimu maalum ambaye anamtafsiria kwa lugha ya kiingereza.
Msuva ameichezea timu yake ya Difaa El Jadid michezo 14 ya raundi ya kwanza kati ya 15 ya Ligi Kuu na amefanikiwa kufunga magoli 5 huku anayeongoza kwa ufungaji akiwa na mabao 8.