Na Mussa Augustine,JamhuriMedia,Dar

Waziri wa nchi ofisi Waziri Mkuu,Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema kwamba nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu zinapaswa kuona kuna haja ya kuwa na uchaguzi huru na wahaki unaozingatia usawa kwa wote.

Waziri Simbachawene alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akifungua wafunzo ya siku nne yakujengea uwezo tume za uchaguzi na wadau wa uchaguzi wa jumuiya ya nchi za ukanda wa maziwa makuu ICGLR.) ambapo mafunzo hayo ni sehemu ya itifaki ya umoja wa mataifa(UN) inayohusiana na masuala ya Demokrasia na Utawala Bora.

Amesema kuwa Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ( ICGLR) zitajadili namna ya kuboresha uadilifu na uchaguzi unaoshirikisha makundi yote katika jamii kama vile wanawake , wazee,Vijana,na watu wenye ulemavu.

Amesema kuwa matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi pia yatajadiliwa,pamoja na fursa zilizopo katika kuboresha ushiriki wa vijana katika uchaguzi ama kama wagombea au wapiga kura ,ambapo pia wajumbe wa mkutano huo uanatarajia kujadili changamoto na fursa zilizopo katika kuborsha suhiriki wa watu wenye ulemavu na wanaoishi kwenye mazingira magumu katika chaguzi mbalimbali.

Waziri Simbachawene ameendelea kusema kuwa Tume za Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa makuu ( ICGLR) zitahakikisha zinaondoa changamoto ambazo zimekua zikisababisha kuwepo kwa siasa chafu na Demokrasi isiyotoa haki sawa kwa makundi yote ikiwemo vijana na watu wenye ulemavu katika kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi.

Amesema kuwa hali ya kuwepo kwa Demokrasia safi husaidia nchi wanachama kuwa na amani na Utulivu kwwenye mataifa yao,hali ambayo pia inasaidia kuondoa vifo visivyo vya lazima vitokanavyo na masuala ya uchaguzi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguizi Tanzania NEC) Dkt Charles Mahera alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uwezo wajumbe na watendaji wa Tume za Uchaguzi za Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.

Dkt.Mahera alizitaja Nchi kumi na mbili Wanachama wa Jumuiya ya ICGLR ni pamoja na Tanzania,Angola,Burundi,Jamhuri ya Afrika ya Kati,Jamhuri ya Kongo,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,Kenya,Uganda,Rwanda,Sudani Kusini ,Sudani na Zambia, zikiwa na lengo wa kuhakikisha chaguzi zinakuwa huru,za haki na zenye kuaminika ili kusaidia kukuza demokrasia itakayochochea amani , Usalama na Ustawi wa Wananchi.