Simba Sc imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji wao Stellenbosch katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali uliochezwa leo Uwanjwa wa Moses Mabhiba jijini Durban, Afrika Kusini.

Simba SC wamenufaika na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa jumapili iliyopitipa kwenye uwanjwa wa New Aman Complex Zanzibar, kwa bao pekee la kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 45 + 2.

Simba sasa inasubiri mshindi wa jumla kati ya RSB Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria ambazo zinarudiana leo kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Mohamed-Hamlaoui Jijini Constantine.