Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Boniface Lyamwike, imeweka wazi majina ya waliopita kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo ambapo wagombea wawili wameondolewa kati ya 21 waliochukua fomu.
Taarifa ya kamati hiyo imewataja waliopitishwa katika nafasi ya Uenyekiti ni wale wale wawili waliochukua fomu ambao ni Swedy Mkwabi na Mtemi Ramadhani.
Katika nafasi ya wajumbe ambapo jumla ya watu 19 walichukua fomu, wawili kati yao wameondolewa na 17 kupitishwa.
Wajumbe waliopitishwa ni:-
1) Hussein Kitta Mlinga
2) Iddy Noor Kajuna
3) Zawadi All Kadunda
4) Mohamed Wandi
5) Selemani Harubu Said
6) Abdallah Rashid Mgomba
7) Christopher Kabalika Mwansasu
8) Alfred Matin Elia
9) Ally Suru
10) Mwina Mohamed Kaduguda
11) Said Tully
12) Jasmine Badar Soudy
13) Juma Abbas Pinto
14) Hamis Ramadhani Mkoma
15) Abubakari Zebo
16) Patrick Paul Rweyemamu
17) Asha Ramadhani Baraka.
Walioenguliwa ni:-
1) Selemani Omari Selemani
2) Omar Juma Mazola
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Novemba 3, 2018. Kwa mujibu wa katiba mpya ya klabu ya mwaka 2018, mgombea wa nafasi ya Uenyekiti anapaswa kuwa na kiwango cha elimu ya Shadaha kutoka Chuo Kikuu.
Katika orodha ya wajumbe watano watakaopigiwa kura, mjumbe mmoja atapaswa kuwa na shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu huku wengine wakiwa na kiwango cha elimu ya kidato cha nne.
Katika hao wajumbe watano mjumbe mmoja anapaswa kuwa mwanamke ili kuleta usawa wa kijinsia katika uwajibikaji wa kazi za klabu.