Klabu ya Simba imepanda kwa nafasi mbili kwenye viwango vya ubora Shirikisho la soka barani Afrika (CAF)
Msimu uliopita Simba ilikuwa nafasi ya tisa sasa imesogea mpaka nafasi ya saba kuelekea msimu ujao
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema ina maana Simba itakuwa kwenye port 2 katika droo ya hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
“Katika draw ya hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika, Simba tutawekwa kwenye Port 2 ambayo inahusisha timu kuanzia nafasi ya tano mpaka ya nane”
“Port A itakua na Al Ahly, Mamelod Wydad na Esparance. Port 2 ndo tutakua Simba na wakubwa wenzetu watatu”
“Brand yetu inazidi kupaaa na Malengo yetu ni kuingia kwenye Port ya kwanza siku chache zijazo,” alindika Ahmed kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii