Baada ya kushindwa kutamba mbele ya Azam FC kwa kupata kipigo chama bao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Yanga imeanza kujipanga na mashindano ya SportPesa Super Cup.
Michuano hiyo inatarajia kuanza Juni 3 mpaka 10 jijini Nairobi nchini humo ikihusisha timu zote zinazodhaminiwa na kampuni hiyo ya bahati Nasibu.
Kikosi hicho kitaanza maandalizi hayo maalum kujiandaa na mashindano hayo ambayo pia watani zake wa jadi, Simba watashiriki.
Klabu ambazo zitashiriki mashindano hayo kwa ujumla ni Simba, Yanga, Singida United na JKU zote za Tanzania, wakati Kenya ni Gor Mahia, AFC Leopard, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys.
Ikumbukwe mshindi wa kombe hilo la SportPesa Super Cup atasafiri kuelelekea England kukipiga na klabu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu England.