Na Isri Mohamed
Klabu za watani wa jadi, Simba na Yanga zinatarajia kuumana kesho katika dimba la Mkapa jijini kwenye mchezo wa nusu fainali ya ngao ya jamii.
Makocha wa timu zote mbili wamezungumza na wanahabari na kuelezea walivyojipanga kuoneshana umwamba katika mechi hiyo ya kufungulia pazia la Ligi Kuu.
“Yaliyopita yamepita huwa sipendi sana kuzungumzia mambo yaliyopita, acha tuone kesho kitatokea nini”
“Hakuna siri kwenye mpira kila kitu lazima kiwe hadharani, kesho ni siku muhimu sana kwani ni mechi ya mtoano, hatupaswi kufanya makosa tunapaswa kuwa makini kwenye kila idara ili kupata matokeo mazuri, naamini mashabiki wetu watajitokeza kwa wingi kwa lengo la kutupa hamasa” Miguel Gamond kocha wa Yanga.
Kwa upande wake kocha wa Simba Fadlu Davies, ambaye hii ni mechi yake ya kwanza ya kimashindano amezungumza haya.
“Tuna vipaji vingi sana kwenye timu, tunaingia kwenye mchezo wa kesho kushinda na bila shaka tutashinda kwakuwa tunachukulia mchezo huu kama michezo mingine na hatuna presha”
Mechi za nusu fainali ya ngao ya jamii zitachezwa kesho Agosti 08, uwanja wa Mkapa, na nyingine ya Coastal Union vs Azam FC itachezwa dimba la Amaan visiwani Zanzibar.