Wekundu wa Msimbazi Simba Sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia katika mchezo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika uliochezwa leo Disemba 15, 2024 katika uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Bao la dakika ya 97 lililofungwa na Kibu Dennis liliihakikishia Simba ushindi na kuibua furaha kwa mashabiki timu hiyo, wakati wakiamini matokeo yangekuwa sare ya 1-1.CS Sfaxien walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tatu, kisha Kibu kuisawazishia Simba dakika ya 7.