Timu ya Klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo a Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na Elie Mpanzu Kibisawala dakika ya 16, Jean Charles Ahoua mawili, dakika ya 21 na 45’+1, Steven Dese Mukwala dakika ya 46 na Kibu Dennis Prosper mawili pia, dakika ya 54 na 69.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 57 na inafikisha pointi 57 ikisalia nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Yanga baada ya wote kucheza mechi 22.

Kwa upande wa Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 27 za mechi 23 sasa nafasi ya nane.